Magufuli ndio Rais ambaye hakuacha legacy yoyote

SGRπŸ˜­πŸ˜…Gani aliacha ? Bila kumaliza wala kichwa cha train hata kimoja

Mradi wa umeme ni uzalishaji, usambazaji yeye kwenye mradi wa umeme yeye alifanya lipo
 
Nadhani legacy ya uongozi wake ni

1.kuwapenda na kuwapigania maskini kiasi cha kuweza kuheshimika hata katika ofisi za serikalini ambazo wasingeweza kuzingatiwa au kujaliwa bila kutoa chochote kitu.

Japo ilikuwa ni nidhamu ya uoga kwa watumishi ili kuogopa kuwajibishwa ila sikumbuki kipindi ambacho hata TANESCO walikuwa on time kama chake.

2. physical infrastructures, alijitahidi kiasi chake kurekebisha masoko, vituo vya mabasi, madaraja, train, mahospitali, majengo ya mahakama etc ambao ulileta mgawanyo wa maendeleo kuliko zamana ambapo kila kilicho kizuri kilijengwa dar. Ndio maana kipindi chake, alidhamiria wazi kuhamisha makao makuu ya nchi kwa kuanzisha na kuujenga mji wa serikali..

3. Inflation rate, kipindi chake alitumia contractionary fiscal policy ambayo hakuingiza pesa kwa wananchi kwa kutokutoa ajira lakini pia kupambana na janja janja za biashara na hivyo kupelekea mfumuko wa bei za vitu kuwa nafuu. Ndicho kipindi japo mzunguko wa pesa ulikuwa mdogo ila bidhaa nyingi hazikupanda kiholela.. Labda uhaba ukitokea kama kile kipindi cha sukari

4. Magufuli alikuwa pan africanist ambaye hakupenda mikataba mibovu tuliyoiongizwa na marais baadhi katika rasilimali zetu. Ubaya alitumia njia ya mabavu kuvunja mikataba ambayo leo ili kurudisha good will na capitalists imebidi nchi ilipe rundo la fedha kisheria...

5. Kiuhalisia aliandaa mazingira ya kulinda rasilimali kiasi hata ujangili ulishuka kiasi cha wanyama kuongezekana na kuvamia makazi ya watu frequently, kitu ambacho kwa sasa hakipo. Lakini pia alitaka gas ya helium na rasilimali ambazo zimegunduliwa hivi karibuni ziingizwe kwenye mikataba fair ili ivinufaishe vizazi vijavyo. Japo sijui ni nini kimeendelea

6. Alipunguza ujambazi kwa kiasi kikubwa na hata vitu vilivyotishia usalama kama case ya kibiti na mtwara vyote aliviweza.. Alikuwa man of his words asieogopa kirahisi


Ana mabaya yake na mazuri pia ambayo siwezi kuyamaliza.. Sikuwahi kuwa fan wake japo kuna vingi vizuri niliviona kwake ila kikubwa alikuwa na clear vision ya Tanzania anayoitaka

So kusema hakuacha legacy, utakuwa unamuonea
 
Unaonaje Hali ilivyo Sasa katika hili bila uwepo wa Magufuri ?
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Kwenye bodi ya mikopo elimu ya juu (heslb) aliweka Retantion fee iliyopelekea wanufaika kulipa adhabu isiyolipika na kupelekea kulipa maradufu.
Maumivu makali nisiyoweza kuisahau kipindi cha awamu ya 5
 
Magufuli aliyechukua elfu ya machinga, aliwasaidia masikini Gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…