Magufuli ndio Rais ambaye hakuacha legacy yoyote

Mkuu wewe ni Mchambuzi wa BBC au VOA? Kwa jinsi nilivyokusoma sidhani kama unatokea Jukwaa la Wahariri.
Wewe akili huna wakati Raisi Trump mwenye VOA anawaona VOA wapumbavu tu na anavunja hilo shirika wewe mndengereko ndio unaona wana akili hopeless wewe

Ona hapa Trump kaibomoa VOA
 
Uchaguzi 2024 wa serikali za mitaa mmepata viti vingapi?

Na huu uchaguzi wa 2025 wa uraisi. Wabunge na madiwani subirini maumivu

Maana wananchi wamekushitukieni kuwa nyinyi ni matapeli tu wa kisiasa
 
Mimi siungi mkono hoja!
Kusema Magufuri hakuacha Legacy yo yote ni kutomtendea Haki kabisa.


 
Miafrika ndivyo tulivyo. Hatujui hata tunataka nini ๐Ÿšฎ

Haiwezekani mtu hata awe mbaya namna gani eti asitende jema hata moja. Naomba uongozi uliopo na ujao uuze kila raslimali tuliyonayo kama taifa - madini, mbuga za wanyama, sijui bandari, ardhi whateva piga bei tu mpaka mitanganyika akili iyakae sawa!

Magufuli alikuwa controversial na kwa aina ya uongozi wake ni wazi alijijengea maadui wengi sana - wale wa vyeti feki, mafisadi na matapeli wa raslimali zetu ambazo alijaribu kuzipigania sana; na wengineo. Na nadhani pia hakupenda kushaurikaa . Tatizo lake kubwa, kwa maoni yangu, ni kwamba hakuwa polished na kuna mambo alitumia nguvu wakati yalihitaji ujanja tu. Kwa mfano, hakukuwa na haja ya kuminya demokrasia vile. Angekuwa mjanja angecheza gemu tu kama anavyocheza mama - very strategic unawaacha watu wanapiga makelele wee huku wakiamini kuwa hiyo ndiyo demokrasia kumbe kimsingi hakuna kitu. Na mambo mengine mengi tu yalihitaji diplomasia dizaini ya Mkwere - anakuchekea kumbe ndiyo anakumaliza!

Angekuwa mjanja pia angejibidisha sana kujua mole aliyekuwa naye pale ikulu ambaye alikuwa anavujisha siri nzito za serikali tena zikiwa za moto. Kikao kinafanyika usiku wa manane lakini kesho yake asubuhi taarifa zote zimeshamfikia dada wa taifa US, Ubelgiji kwa Amsterdam, Norway kwa Ansbert Ngurumo, UK kwa jasusi Chahali; na kwingineko. Sijui kwa nini hali hii aliichukulia poa na nadhani ndiyo ilisababisha anguko lake. Na baada tu ya kwendazake uvujishaji huo wa siri za serikali ukakoma mara moja!

Kwa maoni yangu mimi Afrika hii inahitaji viongozi dizaini ya akina Magufuli au yule dogo wa Bukinabe. Wapate kama 30 hivi halafu wape miaka 30 walipambanie bara hili then waache waende zao. Kutakuwa na maumivu ndiyo lakini watakuachia bara lililovuvumka kifikra na kimaendeleo na ambalo litakuwa tayari kujipambania bila kutegemea matusi na vichambo vya akina Trump.

RIP Mr. President ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ
 
Kwenye bodi ya mikopo elimu ya juu (heslb) aliweka Retantion fee iliyopelekea wanufaika kulipa adhabu isiyolipika na kupelekea kulipa maradufu.
Maumivu makali nisiyoweza kuisahau kipindi cha awamu ya 5
Ninachokumbuka, mama alifuta retantion fee na penalt 2021 na january 2022 nilikuta deni langu limepungua tsh 2.6m ukifananisha na december 2021.
Na hiyohiyo 2021 mama alipandisha madaraja watumishi waliokuwa wamenasa bila sababu.
Mama Alirudisha Ari na morali ya kazi na kuondoa ile fear muda wote.
Anyway mi ni Muoga sana kusema sema mitandaoni, ila huyu mama ikitokea (Mungu aepushe mbali) amefariki, ntakuwa nna msiba wa peke angu achana na ule wa kitaifa.
 
ahaaa ahaaaa ahaaaa unaumwa kweli kweli kukujibu wewe ni kujifaa na mharo mbichi
 
Tutakuwa wawili.
Mimi deni lilishuka toka 14m hadi 8m.
Tofauti ya 6m.
 
Mjinga
 
Kama na wewe ulihesabiwa kuwa sehemu ya watanzania, Taifa limeingia hasara kwa uzao wako.
MAGUFULI ni lidude likuubwa na jina lake litatumika kuombea Kura kwa wana CCM na Wapinzani.
 
Unenena vyema kabisa , alikuwa na mapungufu ya kutumia ubabe , hasa hasa kwenye suala la kujua kucheza double deal mama yupo smart sana kwenye kucheza na maadui zake anakusikiliza hafoki ila anakufinya pole pole na ajisifii kakufinya ahaaaaa
 
Uzi mzuri sana. Uzi ungekuwa takataka kama usingemtaja Shetani Sabaya. Huyo jamaa kafanya maovu mengi sana ambayo hayakufika kwenye media.
 
Yataje hayo mazuri yake
Sgr,Brt phase2,JNHEPP,mafisadi kupungua,kupitiwa upya mikataba ya madini,hospitali nyingi zilijengwa na shule.baada ya kufariki tu miradi ikaamza kutelekezwa na haijaisga Hadi Sasa baada ya awamu ya mafisadi kuingia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ