Magufuli ni Rais wa kwanza ambaye ni zao la mfumo wetu wa elimu kwa 100%

Magufuli ni Rais wa kwanza ambaye ni zao la mfumo wetu wa elimu kwa 100%

Mwenyekiti wetu masomo yake kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kasoma kwa kutumia lugha ya kibeberu, cha ajabu hawezi kujieleza kwa hii lugha. Juzi kati kapigiwa simu na rais wa South Africa kamsakizia polepole aongee naye ndomana tangu awe rais hajawahi kutoka nje ya tz anaona aibu atazungumzaje na marais wenzake.
LOOooo, mkuu 'Blac kid', sijui utafika wapi na mada yako hii!

Umewaza jambo zito sana mkuu, la mfumo wetu mzima wa elimu, jambo ambalo kwetu sisi wengine ndilo tunalodhani kwamba ni uti wa mgongo wa taifa letu.

Sijui kama mada yako hii mhimu itatendewa haki hapa na kujadiliwa kwa kina na upana unaostahiri. Tutaangalia!

Hii ni mada ngumu sana na yenye mihemuko mingi kwa wengine wetu.

Sasa naona kama umetegeshea tu hapo, kwa kumweka Rais Magufuli kama mfano; sasa sijui tujisifu na kujipongeza..., na usisahau, hata akina Museveni walipitia hapa, pamoja na kwamba wameguswa na ya wakoloni pia.

Kipimo changu cha elimu yetu nakiweka kwa kuanzia umri wetu, toka tupate uhuru, miaka inakaribia kwa mtu kustaafu, ndio hawa akina Magufuli sasa.

Miaka sitini, hii elimu yetu imetuletea mabadiliko gani? Tunakwenda mbele au ni kama tunarudi kinyume nyume?

Tumefanya lipi la maana katika muda huo kwa kuitegemea elimu yetu; bila shida naweza kutaja BAKITA - na Kiswahili chetu. Hatuwezi kubeza kamwe kazi kubwa inayoonekana waliyoifanya hawa jamaa.

Kwenye sayansi tumefanya nini? COVID-19 angalia tulichoweza kufanya, ni kipi? Wanasayansi wetu wako wapi? Tunaambiwa tujifukize, mvuke wa kyungu utababwa na kuyeyusha coronavirus; hiyo ni sayansi yetu!

Ngoja nisubiri michango.

Hongera kwa mada makini sana.

N.B. Sijui kilichotokea, lakini 'attribution' kwa mleta mada mkuu 'Ralph Tyler' ndiye lilikuwa lengo langu; pamoja na kwamba kum'quote' mkuu 'Blac kid' kulistahiri pia.
 
Hahaha elimu ya kumfanya muhitimu atimize ndoto yake pia zipo, mfano mzuri SIDO na VETA, sinafundisha mamalishe na mafundi uashi kule, na wakitoka huko wanajiajiri mitaani.

Hivi vyuo vingine vyote wahitimu lazima waajiriwe na Serikali, fikiria rais wetu anayeongelewa hapa asingeajiriwa serikalini angekuwa wapi leo?!
Una uelewa mdogo sana kamanda.
 
LOOooo, mkuu 'Blac kid', sijui utafika wapi na mada yako hii!

Umewaza jambo zito sana mkuu, la mfumo wetu mzima wa elimu, jambo ambalo kwetu sisi wengine ndilo tunalodhani kwamba ni uti wa mgongo wa taifa letu.

Sijui kama mada yako hii mhimu itatendewa haki hapa na kujadiliwa kwa kina na upana unaostahiri. Tutaangalia!

Hii ni mada ngumu sana na yenye mihemuko mingi kwa wengine wetu.

Sasa naona kama umetegeshea tu hapo, kwa kumweka Rais Magufuli kama mfano; sasa sijui tujisifu na kujipongeza..., na usisahau, hata akina Museveni walipitia hapa, pamoja na kwamba wameguswa na ya wakoloni pia.

Kipimo changu cha elimu yetu nakiweka kwa kuanzia umri wetu, toka tupate uhuru, miaka inakaribia kwa mtu kustaafu, ndio hawa akina Magufuli sasa.

Miaka sitini, hii elimu yetu imetuletea mabadiliko gani? Tunakwenda mbele au ni kama tunarudi kinyume nyume?

Tumefanya lipi la maana katika muda huo kwa kuitegemea elimu yetu; bila shida naweza kutaja BAKITA - na Kiswahili chetu. Hatuwezi kubeza kamwe kazi kubwa inayoonekana waliyoifanya hawa jamaa.

Kwenye sayansi tumefanya nini? COVID-19 angalia tulichoweza kufanya, ni kipi? Wanasayansi wetu wako wapi? Tunaambiwa tujifukize, mvuke wa kyungu utababwa na kuyeyusha coronavirus; hiyo ni sayansi yetu!

Ngoja nisubiri michango.

Hongera kwa mada makini sana.

N.B. Sijui kilichotokea, lakini 'attribution' kwa mleta mada mkuu 'Ralph Tyler' ndiye lilikuwa lengo langu; pamoja na kwamba kum'quote' mkuu 'Blac kid' kulistahiri pia.
Elimu yetu ilikuwa inaenda vizuri tu mambo yalianza kuvurugika mwishoni mwa utawala wa the nkapa na liwaziri lake li Joseph mungai na hata tawala zilizofuata zimeshindwa kuirudisha kwenye reli elimu yetu.
 
Mkuu, neno “hii” sio conclusion. Hivi kweli conclusion yako ni “tunayoiona katika kazi za wahitimu wetu”??[emoji15] Kuna kitu hujasema hapa, kiseme tu - una uhuru wa kufanya hivo.
Hata wewe una uhuru wa kusema. Sema tu.
 
Kwani JK alisoma wapi..? Kwa taarifa tunazozijua JK naye pia amesoma hapa nchini kuanzia elimu ya msingi,sekondari hadi chuo kikuu cha Dar as salaam hivyo JPM sio wa kwanza alietokea katika mfumo wa elimu wa Tanzania.
JK alianza elimu ya msingi wakati wa Tanganyika ya ukoloni akamaliza chuo kikuu Mlimani ndani ya Tanzania huru ya Nyerere, kwa hiyo amechanganya elimu za mfumo wa kikoloni na ule uliofuata wa Nyerere. JPM amesoma hatua zote ndani ya Tanzania huru.
 
Kumbe elimu yetu inatakiwa kufanyiwa marekebisho!.
 
Ndiye Rais pekee wa Tanzania ambaye amepata elimu yake yote katika Tanzania huru kwa mfumo wa elimu wa Tanzania katika hatua zote. Waliomtangulia wote walipitia mfumo wa elimu ya kikoloni kwa hatua mbalimbali.

Hongera kubwa sana ni kwa Mwalimu Nyerere ambaye alisoma katika mfumo wa elimu ya kikoloni kwa 100% lakini ndiye aliyeasisi mfumo wa elimu ya Tanzania huru, hadi leo hii tuna Magufuli kama zao la elimu yetu wenyewe kwa 100%.
Unaona sasa?

Hii haikuhitaji utabiri. Mada imedoda!

Mkuu Ralph Tyler, wewe mwenyewe umehusika pia kuiua. Ulitakiwa ui'moderate' mada yako badala ya kutegesheza tu kama ulivyofanya. Yaani uko 'vague' hata haijulikani umesimamia wapi - kama unabisha, angalia mistari yako hiyo minne uliyoweka hapo!
 
Acha uchokozi.
Changia mada kama unacho cha kuchangia.
 
Acha uchokozi.
Changia mada kama unacho cha kuchangia.
Nilidhani unao ufahamu fulani juu ya mada ile, kwa hiyo nilikuwa na matumaini sana kuona itakavyokwenda.

Ni mada muhimu sana mkuu, lakini naona kama hukuichangamsha mbali ya kuweka mistari hiyo tu isiyo na mwelekeo unaoonekana.

Basi tuliachie hili hapa, kwani haliongezi chochote juu ya mada yenyewe.
 
Back
Top Bottom