Elections 2015 Magufuli: Nikifanikiwa kuwa rais nitakulinda kwelikweli Diallo

Elections 2015 Magufuli: Nikifanikiwa kuwa rais nitakulinda kwelikweli Diallo

MLALUKO JR

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2015
Posts
962
Reaction score
309
Ndugu wana-JF habarini.

Mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu, mnalichukuliaje suala la mgombea urais kupitia CCM kumwambia Antony Diallo kuwa atamlinda saaana kupita maelezo pindi atakapoingia Ikulu?

Ndugu zanguni imekaaaje hii, kwa kiongozi kutamka hivyo mbele ya wa wana-CCM na Wa-tz kadhaa bila aibu!?
 
Anasema ataunda mahakama ya mafisadi na kupambana na ufisadi wakati huo huo akiasisi mafisadi wapya!
Fuatilia ahadi zote za Mkagufuli hakuna hata moja yenye time frame kama wengine wanaosema siku 100, siku 21, mwaka mmoja nk. Mfano angelisema hiyo mahakama ataiunda baada ya siku ngapi kuanzia Oct 25 tungelimuelewa maana karibia 90% ya alikuwa nao pale Jangwani jana ni mafisadfi papa.
Wizi wa kura utafanyika lakini tukipiga kura kwa umakini tunaweza kuibadilisha taasisi ya urais na kuipa hadhi inayostahili hapo kesho!
 
Star CCM TV inampigania ucku na mchana,mahojiano maalumu kila muda,clip za kuedit.Nawashukuru WaTZ wamestuka,wameona haitoshi wanapeleka matangazo ya biashara ya mgombea wao ITV Lakini wapi
 
Atamlinda kwa kuwa Star TV imekuwa ikifika sheria, maadili, na weledi ktk fani ya Habari. Kwa kutamka hivyo, Magufuli anajua kuwa Star Tv inapaswa kuadhibiwa.

Sasa wenye akili ndio tujue kama Dk. Magufuli anaweza kweli kuleta mabadiliko ya Utendaji ktk CCM na Serikali, ama la.

Vv
 
Anthony Dialo ni mwekezaji namba moja kanda ya ziwa. Anamiliki vitega uchumi vingi na ametoa ajira nyingi kwa Watanzania kama alivyo Bakhressa, Manji, Dewji nk. Kubwa zaidi, ni Anthony Dialo pekee ndiye aliyejitolea kumtetea na kumlinda Magufuli kwenye kampeni zake pale alipoamua kurusha moja kwa moja matangazo ya mikutano ya Magufuli.

Ningemuona mtu wa ajabu sana kama asingeliona hilo. Reginald Mengi na Rostam Aziz aliweka azma ya kutorusha taarifa za Magufuli na kumpa muda wa kutosha Lowassa.

Big up Magufuli. Mlipe fadhila anayekutendea wema. Ikiwa Dialo atadhurika, atasababisha ukosefu mkubwa wa ajira
 
Atamlinda kwa kuwa Star TV imekuwa ikifika sheria, maadili, na weledi ktk fani ya Habari. Kwa kutamka hivyo, Magufuli anajua kuwa Star Tv inapaswa kuadhibiwa.

Sasa wenye akili ndio tujue kama Dk. Magufuli anaweza kweli kuleta mabadiliko ya Utendaji ktk CCM na Serikali, ama la.

Vv
Vipi kuhusu TV zenu za ITV na Channel Ten?
 
Ndiyo maana ya CCM ni ile-ile, na urasimu ule-ule.
Ni wakati wa mabadiliko.
 
Ndo maana hatashinda. Hizi tabia zakulindani ndo zimetufikisha hapa leo na maendeleo kiduchu kuliko uwezo wetu.

Ni tabia hizihizi ndo maana watu wanakwepa kodi. Kauli za hovyo sana hizi kutoka kwa kiongozi.
 
Magufuri hafai hata chembe.kumchagua magufuri ni kuitumbukiza nchi chooni.utawala wake utakuwa wa upendeleo na kulindana tena kuliko utawala unaomaliza muda wake.ni hatari kumpa uraisi.
 
Hii imemshushia hadhi Magufuli kwa kuwa Diallo sio mtu muadilifu sana na rafiki wa kweli wa watanzania.Huyu jamaa hana tabia ya ku-calculate matamshi yake.Anapaswa kubadilika.
Ndugu wana-JF habarini.

Mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu, mnalichukuliaje suala la mgombea urais kupitia CCM kumwambia Antony Diallo kuwa atamlinda saaana kupita maelezo pindi atakapoingia Ikulu?

Ndugu zanguni imekaaaje hii, kwa kiongozi kutamka hivyo mbele ya wa wana-CCM na Wa-tz kadhaa bila aibu!?
 
Vipi kuhusu TV zenu za ITV na Channel Ten?

Wanawapendelea kina nani kinyume na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari? Sijaona ITV mahali wamempendelea mgombea mmoja dhidi ya wengine. Na mbona mikutano ya CCM pia imewahi kurushwa moja kwa moja na hivyo vituo. Labda wao hawataki kukopwa kama Star Tv.

Vv
 
Namshangaa sana Dkt.Magufuli kwa kutoa ahadi za kukurupuka
 
Anachofanya Diallo ni kutoa rushwa kwa Magufuli ili kama atapata kuwa Rais, aweze kupata "privileges" kwenye biashara zake e.g. misamaha ya kodi. Na anachomaanisha Magufuli ni kwamba wafanyabiashara ambao hawajachangia kampeni zake "hatawalinda". That is a real political gaffe (when a politician tell the truth in public he isn't supposed to say). You could see Magufuli is not that intelligent anyway.
 
Ataja kuwa rais hatari na wa visasi hafai hapo bado migomo ya madactari,manesi,waalimu,wanafunzi je itakuweje.
 
kama watu wasio na nia njema wanataka kumudhuru kuambiwa hivyo ni faraja na siyo dhambi
ww tuu umefasiri vibaya
 
Back
Top Bottom