Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Mawaziri wa juu ni wale wanao jiandaa kugombea urais, na kwa maana hiyo hapo ni eitha alikuwa ana mtwanga JK au Eddo.
Sasa kama hakukuwa na ushahidi kuwa ni mawaziri walimpa sumu bali hisia zake na ukweli ni kiporo alichopewa na mama jeska basi amesha jenga ugomvi mkubwa sana na mawaziri walio kuwa katika baraza wakati huo.
Nina hakika habari hizo (za sumu) hazikuwepo katika hotuba aliyo tayatishiwa bali kwa tabia zake kachomeka tuu!
 
Reactions: rr4
Binafsi nilishitushwa sana na Kauli ya Jana ya Mhe.Rais kuwa aliwahi wekewa sumu baada ya kupongezwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Nimejiuliza maswali mengine sana.

Je!inawezekana wenyewe kwa wenyewe wanapowekeana sumu wasio wa kwao wanapotezwa kama Azory,Ben saanane?

Je!inawezekana wenyewe kwa wenyewe wanapowekeana sumu wasio wa kwao wanapigwa Risasi kama Lissu?

Je!inawezekana wenyewe kwa wenyewe wanapowekeana sumu wasio wa kwao wanatekwa kama Mo,na wengineo?

Je! Inawezekana wenyewe kwa wenyewe wanapowekeana sumu wasio wa kwao wanauawa kama Mawazo?

Kuna Maswali mengi sana ya kujiuliza lakini pia maswali haya hayana majibu.
Lakini swali la mwisho la kujiuliza ni hili,Hii Amani ya kweli ya nchi yetu kama tunavyoimba kwenye wimbo wa Taifa,au tunaimba kwaajili tu ya kuifurahisha Dunia? Mungu atunusuru na haya.kama kweli Dhamiri zetu zimekufa kiasi hiki hata kuchakachua uchaguzi nini kitatushinda?
 
Chadema walitaka kumteka na kumuua mstahiki meya Jacob wa ubungo.

Ufipa kuna watu hatari na wabaya sana!
 
Inawezekana ikawa kweli, lakini kwa jinsi JPM anavyoendesha siasa, kwangu inakuwa vigumu kumwamini.
 
Inawezekana fitina na madhila kwa ex pm wa Ben ni mwendelezo kulipia visasi. Mbali ya kuwa alijiunga na upinzani.
 
Unajuaje mtu anakuonea wivu bila kukufanyia jambo baya au kufanya kitendo Cha kukudhuru?
 
*Classified* information ni zile ambazo ni "top secret, confidential ama secret " sasa hii ishatoka huko imekua *unclassified* inaeza jadilika
 
Chadema walitaka kumteka na kumuua mstahiki meya Jacob wa ubungo.

Ufipa kuna watu hatari na wabaya sana!
Cha kushangaza Wewe unawajua hao watu hatari lakini umekaa kimya huendi kuwaripoti polisi.Kukaa kimya inaonyesha Wewe ni hatari zaidi.
 
Hata Mh. Kikwete alisha sema CCM ilifika mahali huwezi kukaa na wenzako ukaacha glass ya kinywaji chako na urudi ukinywe, hawa watu wana tamaa ya madaraka wako tayari hata kusababisha mauaji ya kimbari ili mradi wabaki madarakani.
 
Hata chachawangwe ni yalele yale wao kwa wao...
 
*Classified* information ni zile ambazo ni "top secret, confidential ama secret " sasa hii ishatoka huko imekua *unclassified* inaeza jadilika
Nilichoona mimi, ni kwamba amekuwa too much specific kwenye declassification ya hili jambo. Hajaacha utata hata kidogo. Na sawa na kusema kiongozi wa juu katika nchi. Kuna mwingine zaidi ya Rais? Declassified zinatakiwa kuacha utata kidogo ili kuepuka harm or hurt or humiliation kwa baadhi ya specific individuals.
 
Mungu aendelee kumlinda "John"
Kumbe kuna watu wenye busara walishaliona hili linakuja kuwa tatizo kubwa wakataka kuliondoa mapema. Sema sumu feki alipewa lofa hasiyejua kuichanganya vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…