Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Uko sahihi huyu mzee huwa ni muongo haijapata kutokea

..inawezekana alipata food poisoning, yaani alikula chakula kibaya, halafu yeye akaamini kuwa amelishwa sumu.

..kama aliwekewa sumu then hatua gani zilichukuliwa? Na yeye sasa hivi si Raisi nini kimemzuia kuchukua hatua?

..Magufuli ambaye ukimkosoa anaona umemtukana anaweza kweli kumvumilia mtu aliyemlisha sumu na kutaka kumuua?
 
Hivi CCM kuna nini kila mtu sumu lakini sisi wengine risasi CCM ni janga la taifa

CCM ilifikia wakati jinsi wasivyoaminiana ,kila mmoja alikuwa anaingia na chupa yake ya maji mkutanoni!!!
 
Pls spare my ribs jaman..had nimechoka kucheka jaman
Mtu umeshakuwa maarufu, lakini bado unatafuta umaarufu, ili iweje?!. Alinyweshwa sumu ya aina gani? nani alimnywesha?.

Yeye alikuwa ambitious kama binadamu wengine, akakanyaga wenzake, na alifahamu kawakanyaga .

Sasa akaingiwa woga, mtu wa aina hiyo hata akijikwaa kawaida atasema karogwa.
 
Hilo tukio la kunyweshwa sumu la mzee Magufuli, lina akisi sehemu ndogo tu ya roho ngumu na michezo ya kila siku ya hao wanasiasa, mbali ya uchawi, ni wakatili msiwaone hivyo.
Kumbuka tukio la Lissu, na viongozi wengine waliopotea katika ajali za kutatanisha.
 
Rais Magufuli akiwa kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mzee Benjamin Mkapa amefunguka mambo makubwa mno hajawahi kuyasema popote, mambo aliyoyasema ni pamoja na utendaji kazi wake uliomkosha Mzee Mkapa, Kuchukiwa na mawaziri na viongozi wengine wakubwa mpaka kunyweshwa sumu nk

Magufuli amepita majaribu Mengi hadi kufikia kuwa Kiongozi wa Nchi

Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu Mzee.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWA UFUPI

Nampongeza Mzee Mkapa kwa kutimiza miaka 81, Mzee Mkapa ni shujaa wangu naomba nitayozungumza leo yasitafsiriwe vibaya na kupotoshwa.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge, mzee Mkapa aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi chini ya Mama Anna Abdallah, hata sikujua kwanini aliniteua, lakini nazidi kukushukuru mzee Mkapa

Moja ya mambo akifurahia jambo hafichi furaha yake na akichukia hafichi chuki yake, nakumbuka Mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri alipata furaha sana kwenye kazi za barabara mpaka akatamka kuwa mimi ni Askari wake namba moja.

Nilichojifunza kwa Mzee Mkapa ukimshauri kitu na kikitekelezwa hata yakitokea makosa hatakuacha peke yako atasimama na wewe

Wakati nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na nitoe siri leo, makatibu wakuu wengi hawawaheshimu manaibu waziri, lakini nilipokuwa natoa maagizo yalipokuwa hayatekelezeki, mzee Mkapa alikuwa anatoa maagizo yeye na maagizo hayo yanatekelezeka

Nilipofanya kazi vizuri Mzee Mkapa hakusita kunisifia na sitosahau siku aliyotangaza kuwa, Mimi (Magufuli) ni askari wake wa mwamvuli, baada ya kutangazwa hivyo nilichukiwa na Viongozi wengi akiwemo wa ngazi za juu hadi kufikia hatua ya kunyweshwa sumu Dodoma

Nashukuru Mungu baada ya kunyweshwa sumu na kupona, nilienda kwa Mzee Mkapa na kumueleza azma yangu ya kujiuzulu, nakumbuka aliniangalia kwa jicho la mama na mwana na kuniambia usijiuzulu akanipa ulinzi na kuendelea kuchapa kazi

Nilichojifunza kwake Mzee Mkapa ni mtulivu, Mcha Mungu, mwanadiplomasia, mwanafunzi wa Sera na falsafa za Mwl. Nyeyere, asiye mnafiki na msema kweli

Niwahimize viongozi wastafau kuandika vitabu, nafurahi kusikia vitabu vya Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi vipo katika hatua za mwisho kukamilia, hili lisiishie kwa Marais wastaafu, ningefurahi kusikia Maalim Seif akaiandika kitabu, Mzee Warioba na wengine wakiandika.

Alilishwa sumu ya aina gani...aseme kama ni Cyanide au ni nini? Hayo mambo ya kusema " Nililishwa sumu" au "nililogwa " au nini sijui halafu unashindwa kutoa details huo ni uongo mtupu, Alikuwa na ugonjwa wake ambao hataki kuusema aache uongo au kusingizia. Hatua gani ilichukuliwa baada ya yeye kulishwa sumu??? Au ndiyo anawalipizia akina Lissu, Ben Saanane, Azzory na wengine anaoendelea kuwapoteza. HAYO NI MANENO YA MKOSAJI....Magonjwa yako yanafahamika tangu ulivyokuwa unaenda kwa babu wa Loliondo
 
Kitabu cha Mkapa sasa topic za kiki za nini. Kila mtu anataka yeye ndiye aongelewe sad mpeni mzee Mkapa heshima yake
 
Alilishwa sumu ya aina gani...aseme kama ni Cyanide au ni nini? Hayo mambo ya kusema " Nililishwa sumu" au "nililogwa " au nini sijui halafu unashindwa kutoa details huo ni uongo mtupu, Alikuwa na ugonjwa wake ambao hataki kuusema aache uongo au kusingizia. Hatua gani ilichukuliwa baada ya yeye kulishwa sumu??? Au ndiyo anawalipizia akina Lissu, Ben Saanane, Azzory na wengine anaoendelea kuwapoteza. HAYO NI MANENO YA MKOSAJI....Magonjwa yako yanafahamika tangu ulivyokuwa unaenda kwa babu wa Loliondo

🤣🤣🤣umebold mbaya🤣🤣🤣🤣..huyu hanaolote ni attention seeker!sijui yukoje tu
 
Imeniuma sana kusikia kuwa Rais wangu alipitia jaribio kubwa kama hilo!
ama kweli baadhi ya binadaamu ni wabaya kuliko wanyama. Watanzania acheni kuoneana wivu makazini, acheni chuki, acheni majungu, acheni fitina na unafiki, haya mambo ndio yanawaumiza wengi.

Pole sana Rais wetu mpendwa, tunakuombea Mungu aendelee kukulinda daima! Viongozi wote hakikisheni mnaondoa majungu na fitina kazini kwani mambo hayo huzaa uadui.
 
imeniuma sana kusikia kuwa Rais wangu alipitia jaribio kubwa kama hilo!
ama kweli baadhi ya binadaamu ni wabaya kuliko wanyama.

watanzania acheni kuoneana wivu makazini, acheni chuki, acheni majungu, acheni fitina na unafiki, haya mambo ndio yanawaumiza wengi.

Pole sana Rais wetu mpendwa, tunakuombea Mungu aendelee kukulinda daima!

viongozi wote hakikisheni mnaondoa majungu na fitina kazini kwani mambo hayo huzaa uadui.

Acha uzandiki ww!kama hujui sanaa kaa kimya!huu uzi ni wa kaole sanaa group!
 
Back
Top Bottom