Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Kama yule jamaa ! Badala ya kupiga mtu zote 19 anapiga kwenye mlango wa Land Cruiser ! Hovyo sana.
Hata JKT hajapita kashika SMG kaachia moja kasikia mlio miguu, mikono yote kitete ; Mtu asiye na akili hata busara huwa hana... execution ikawa incomplete yaani below 15%; majibu kwa wakubwa zake hayapo inabakia aibu tupu.
 
Nakumbuka Magufuli kupewa ulinzi lakini wakati ule tulidhani ni kwa sababu ya magari ya serikali. Ninachoomba ni nani hasa hao mawaziri waliopenda kusifiwa wao hadi kumpa sumu mwenzano? Ngoja niangalie baraza la mawaziri la wakati ule.
 
Kwa tunaojua na kufatilia mambo ya siasa ni kweli huyu Mhe. Wakati ule alilishwa sumu. Na alipelekwa kutibiwa Ujerumani. Baada ya kurudi alipewa ulinzi wa uhakika. Na ikawa ngumu tena kumuona Magufuli akijichanganya kama zamani. Swala hili kwa wakati huo alikuenea sana kwani hakukuwa na vyombo vingi vya habari kama sasa. Ila kwa wale tuliokuwa tukifuatilia siasa za wakati huo kwa karibu tulizipata hizo nyepesi nyepesi.
Wahusika ni wakina nani? watu gani hao wakubwa waliompa sumu huyo Magufuli? Haitoshi kusema tu alilishwa sumu, awe specific, aina ya sumu, muda, alitibiwa wapi na wakubwa hao waliohusika walichukuliwa hatua gani. Otherwise hiyo ni hoax tu.
 
Majuzi zote tumemsikia Mhe Rais kupitia hotuba yake na kupitia vyombo vya habari kuwa enzi akiwa waziri alinyweshwa sumu na viongozi wenzake waliomeonea wivu.

Pia alidai kuwa baada ya kupona alimkabili Rais wa wakati huo Mkapa, kumkabidhi barua ya kujiuzulu.

Maajabu ni kuwa Rais Mkapa hakuhangaika kuchunguza wala kuchukua hatua yoyote zaidi ya kumwambia amtangulize Mungu na kuendelea na kazi.

Maajabu haya yanaleta shaka kubwa sana kwa upande wa taasisi kubwa kama Rais kukalia kimya tuhuma za majaribio ya mauaji kwa kutumia sumu.

Ningekuwa mimi ningewaleta hata FBI kusaidia.

Swali langu, ni kwanini hatuambiwi hatua za kiuchunguzi zilizochukuliwa? Kwani watanzania hatuna haki ya kuwajua wahusika? Kwanini viongozi wanatuchukulia kama watu wasio na msaada wala uelewa wowote?

Nawasilisha.
 
Unajuaje ni humo humo. Nafikiri unaelewa .Amchunguze nani tena. Waliolishwa Mawaziri kwani ni yeye au ni wengi sijui inawezekana walichunguza .
 
Kumbe hata vifo vya Komba na Balali huenda ni michezo? Hata hivyo yeye sasa ni rais hana haja ya kumwogopa mtu awataje na wafanyiwe uchunguzi na kushtakiwa kwa kutaka kuua
Komba kumsapoti Lowasa ndio kulimgalimu alikua na deni kubwa CRDB bank baada ya kutamka anamsapoti lowasa tu kwenye kile kipindi cha eatv cha salama walikua wanaita mkasi nazani da CRDB wakapewa maelekezo ha ha ha ha ha trela wakataka kuuza kiwanja chake nazani kina petrol station aliweka kama dhamana wakati huo shule yake ya bakili muluzi nayo inaandamwa na madeni na haifanyi vizuri kupiga simu kwa PM amsaidie holaaa mzee presha juu dakika sifuri akakata moto wakampeleka TMJ pale story ikaishia hapo
 
Daaah sijui sumu walichukua duka gani maana ndio inayotusababishia haya matezo Leo
 
Uzinduzi wa Kitabu cha Mkapa uliingiliwa na jinamizi jipya la hadithi ya Waziri wa JMT kulishwa Sumu na waziri/mawaziri wenzake wa JMT kwa vile tu aliitwa askari shujaa wa miavuli wa awamu ya tatu.
Wanasheria wangesema tukio la Mkapa has been taken by event.

Kashkash za JPM kuenea kwamba kanyweshwa Sumu na baadae kapewa ulinzi tulizisikia na nakumbuka nikiwa civil servant, story hizo zilizagaa kwenye makorido ya ofisi nyingi za serikali.

Lakini kwa kumbukumbu zangu BM alipotoa ulinzi kwa JPM haikuwa kwa vile eti kapewa Sumu na mawaziri wenzake bali lilikuwa ni tishio na amri aliyo itoa JPM ya magari ya miradi ya wafadhili kutotumia namba binafsi kwani wengi walijibinafsishia magari hayo bila hata serikali kujua na ndipo ukaja usajili wa namba DFP kwa magari ya miradi.
Hiyo hadithi ya mawaziri wenzake kumpa Sumu nadhani imeingizwa pale kwa makusudi maalumu na ndio maana ilipokelewa kwa nyuso za mshangao na baadhi ya mawaziri wa zamani akiwapo JK.

Jee nini lengo la tuhuma hizo nzito kusubiri na kuzitoa hadharani kwenye kilele cha tukio jingine?
Tukubaliane kwamba tukio la kumuwekea Sumu mtu mwingine ni jinai na sheria inafuata mkondo, jee liliishaje hilo wakati JPM alikwisha jua kuwa mawaziri (lazima aliwajua kwa majina) wamemuwekea sumu?
Kama njama za kumuua waziri na zinafanywa na mawaziri wenyewe nchi ilikuwa imefikia kiwango cha juu cha uhalifu na Rais Mkapa alishindwa kulishughulikia hilo?

Ndio maana nafikiri sinema ya igizo hili haikuchezwa sawasawa kwani imezalisha maswali badala ya kuleta majibu au burudani. Mawaziri wa 1995-2005 wamevunjiwa heshima mbele ya jamii kuwa walikuwa na wivu kwa mwenzao na ni wauwaji.

Au ni washauri wa Rais ndio wameshindwa kuusoma mchezo kuwa una madhara?
 
Aisee sijaoata kuona kiongozi mwongo kama Jiwe!

Hivi yeye alishwe simu, suala lake liishe kimya kimya!

Mbona wakati ule Waziri Mwakyembe alipojipangusia taulo yenye sumu, tulitangaziwa Taifa zima??

Na tunaona jinsi sumu hiyo ilivyomuathiti kwa kunyonyoka nywele kichwani mwake

Swali la pili, hivi kweli unaanini kama hao watu wangekuwepo duniani, kwa namna anavyoendekeza siasa ya chuki??
 
MOD mumeichanganya thread yangu humu na imepoteza maana kabisa.
Sawa hata nikitiririka uzoefu wa yaliyotokea wakati huo na hii hadithi ya kupewa sumu hayataleta maana zaidi ya kuwachanganya.
Basi acha nipotezee tuu ili mufurahi
 
Chakaza,
Mkuu, hizi siasa zina mengi ya chini ya kapeti ambayo huifikia jamii kwa njia ya minongono ya mitaani.

Nasikia mhusika mkuu ni yule ambaye alimuachia jimbo Mama mmoja hivi anavaa mawani na ni mwanaharakati wa haki za kinamama.

Wote wawili wanatoka lile eneo ambalo ukiwa unataka kukata kona kuelekea mto wa mbu kama unatoka Arusha, basi haukati kona unaendelea mbele.

Mitandao ya JK na ENL ilitaka kutupeleka pabaya, maslahi ya kisiasa na yale ya binafsi hayakuwa na lengo zuri kwa taifa hili.
 
Mkuu, hizi siasa zina mengi ya chini ya kapeti ambayo huifikia jamii kwa njia ya minongono ya mitaani.

Nasikia mhusika mkuu ni yule ambaye alimuachia jimbo Mama mmoja hivi anavaa mawani na ni mwanaharakati wa haki za kinamama.

Wote wawili wanatoka lile eneo ambalo ukiwa unataka kukata kona kuelekea mto wa mbu kama unatoka Arusha, basi haukati kona unaendelea mbele.

Mitandao ya JK na ENL ilitaka kutupeleka pabaya, maslahi ya kisiasa na yale ya binafsi hayakuwa na lengo zuri kwa taifa hili.
Kukosana kwa JK na ENL ilikuwa divine intervention kuliokoa taifa.
 
Mkuu, hizi siasa zina mengi ya chini ya kapeti ambayo huifikia jamii kwa njia ya minongono ya mitaani.

Nasikia mhusika mkuu ni yule ambaye alimuachia jimbo Mama mmoja hivi anavaa mawani na ni mwanaharakati wa haki za kinamama.

Wote wawili wanatoka lile eneo ambalo ukiwa unataka kukata kona kuelekea mto wa mbu kama unatoka Arusha, basi haukati kona unaendelea mbele.

Mitandao ya JK na ENL ilitaka kutupeleka pabaya, maslahi ya kisiasa na yale ya binafsi hayakuwa na lengo zuri kwa taifa hili.
Umeniachia chemsha bongo Kali, ngoja nirudi kusoma tena maana umenitoa kabisa kwenye track!
Ila ni kweli hali ilikuwa mbaya sana hata yale alisema JK kuhusu kuacha maji mezani yalikuwa kweli.
 
Back
Top Bottom