Uchaguzi 2020 Magufuli si mgombea wa Tanzania pekee bali Afrika nzima inamuhitaji

Mleta mada usitufanye wote wapuuzi humu

1. Yani kwa akili yako sifa ya Raisi ni Mtu ambaye haendi Ulaya na America????

2. Kwa akili yako unafikiri mtumishi akisafiri nje ya nchi ndo hatumikii wananchi??? Unajua Safari za nje ya nchi zinakuwaga za aina gani na malengo gani??? Au unafikiri watu wanaenda vacation tu???

3. Nani kakwambia magufuli anatumia wasomi kwa maendeleo ya nchi??? Anawaburuza wasomi au anawatumia kwa maendeleo ya nchi??? Unajua Msomi Prof Assad alifanywa nini na huyo Magufuli???

4. Unasema kafufua shirika la ndege kwa kununua ndege! Labda nikuulize unajua financial statements za Air Tanzania wewe??? Unajua mchakato wa kuuziana izo ndege ukoje???

5. Hivi unajua hali za kifedha za hayo mashirika yanayotoa gawio??? Nakushauri nenda kafuatilie financial statements za ttcl uone kama linajiendesha kwa faida, fuatilia hayo mashirika mengine kama national housing , ppf, nsssf kama yanajiendesha kwa faida??

6.Unazungumzia uwajibikaji gani wa viongozi wa umma??? Makonda alikutwa na vyeti feki alimwajibisha????

7. Tuliambiwa tunawadai acasa trillion 490???? Unajua zilipotelea wapi??? Uliwai kuhoji???

8.Ni miundombinu gani ya ameboresha yeye?? Hujui kuwa asilimia 95 zilikuwa project za JK. Au unasema uwanja wa kijijini kwake Chatto ambao hata zabuni yake hatuijui???

9. Bima ya afya gani ameboresha wakati kapunguza hadi magonjwa ya kuhudumiwa na Bima???

10. wachezaji gani wananufaika??? Hujui hata Ligi kuu kuna wachezaji hawalipwi mishahara miezi na miezi????

11.Heshima gani ya Tanzania imerejea?? Kuwa na Urafiki na wafu Burundi na Zimbabwe au????

12. Kilimo gani kimeimarishwa??? Hujasikia malalamiko ya wakulima wa Korosho, Mbaazi, Tumbaku na Mahindi??? Au unaishi Misri????

13. Imani gani ya wananchi imeongezeka??? Au watu wamenyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao kutokana na kubambikiwa makesi, kupigwa risasi na kupotezwa pale wakitoa mawazo yao huru???

Kajipange upya kilaza wa Lumumba wewe!!!
 
Magu ameleta vurugu kubwa Africa Mashariki, alipomaliza akaenda SADC nako kavuruga leo nimesikiliza redio Namibia wanamchamba vibaya kwa amekuwa akiwaaminisha watu wake corona haipo na hataki kutoa ushirikiano na nchi nyingine za SADC. Tuna kiongozi wa hovyo sana na naona jinsi nyie timu masifu mnavyopata shida kumsifia mtu huyu, ukweli ni kwamba hakubaliki.
Sema wewe ndo unamhitaji
Hatuhitaji muaji hata kama angekuwa anagawa maziwa na asali bure
Ameua nani weka ushahidi ukishindwa usiandke kwa ushabiki
Magufuli hamna Mkenya anayemuhitaji
We haumuhitaj
Hata yeye hawaitaj wakenya
Weka ushahidi kwamba si muuaji
 
Baada ya October 28 takutafta tumuone anaekubalika
 
Acha kujishebedua ww
 
15. Kuimarisha huduma za afya na Bima ya Afya, sasa hivi wenye bima wanapokelewa kama wafalme hospitalini, zamani tuliwekwa benchi
Mkuu hapa kwenye BIMA ya afya hasa kwenye madawa na baadhi ya huduma kama vipimo wamevurunda sana kwenye mabadiliko waliyofanya karibuni kipindi cha Magufuli.

Kama tunampenda naomba tuwe wakweli kuhusu jambo hili la NHIF, na mengine ambayo kwa hapa nayaweka pending.
 
Me nawasubir baada ya October 28 niwaone
Kwa hizo propaganda zake za maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu labda achaguliwe na wakimbizi.
Huku mtaani hari ya maisha ni mbaya kupindukia.

Mwambieni huyo jiwe wenu (yesu wa CCM) aende kuomba kura flyovers, burigi National Park, Chato International Airport, n.k ila sio raia wa Tz maana njaa iliyopo mtaani sio ya kitoto.
 
Umenifurahisha kwa kumpa ukweli wake mbulula anayetaka kuwafanya Watanzania wote akili zao kama zake na wenzake hapo Lumumba.
Hivi nani asiyejua jinsi awamu hii ilivyotutoa kwenye heshima kimataifa na kikanda hadi kuwa taifa lisilo na hadhi?
Juzi tuu tumefiwa na mzee wetu Mkapa ambaye umaarufu wake ulivuka mipaka ya EAC, SADC na AU hadi kule alikokuwa mwenyekiti mwenza lakini ona response ya majirani na marafiki zetu katika msiba?
Tumedharaulika sana, tena sana tuu
 
Wahuni hawa ndugu. Wameishi kwa propaganda kwa miaka 5 sasa wanafikiri watanzania wote ni mamburula. Subiri tuwaonyeshe kuwa tuna majibu juu ya propaganda zao zote kwa sababu tunaijua Tanzania imetoka wapi?? Ipo wapi na inaenda wapi???
 
Mwambie huyo mataga mwenzako. Anafikiri watanzania ni mamburula kama yeye!
 
Mwambie huyo mataga mwenzako. Anafikiri watanzania ni mamburula kama yeye!
Mkuu ukiniita MATAGA unanikosea heshima japo hatujuani.
Anyway unayo haki kuita yeyote jina lolote lakini hakikisha hauvunji sheria, haukandamizi haki ya huyo mtu.
Kwa hapa umekandamiza haki yangu.
 
Baada ya October 28 takutafta tumuone anaekubalika
 
Kuongoza afrika kuna hitaji akili na sio nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…