Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MAGUFULI SITAKUCHAGUA, WEWE ULE BATA, MIMI NISOTE.
Na, Robert Heriel.
Haya ni maamuzi yangu, wala sitaki mtu ayaingilie. Nimeamua kwa akili zangu. Bahati njema mimi sio Mnafiki, nyeupe ni nyeupe, Nyeusi ni nyeusi.
Mimi sio mtoto mdogo, sio mjinga. Naishi leo, sidanganyiki na kesho. Hayo mambo ya kuniambia maisha mazuri yatakuja kesho wanaambiwa wajinga. Hakuna maisha mazuri kesho. Maisha ni leo. Tunaishi leo, tunafurahi leo, tunakula bata leo.
Wewe ule bata leo alafu unambie mimi nile bata kesho, thubutu! Mimi sio Mjinga.
Magufuli watakuchagua hao hao wapenda maisha ya kesho, ila mimi Taikon, kama Mungu aishivyo siwezi kukuchagua. Yaani unidanganye kama mtoto nami nikuchekelee., Wewe ni nani ujuaye kesho kama sio kudanganyana.
Linalowezekana leo lifanyike leo, mambo ya kesho hayanihusu, na sitaki yanihusu. Ikifika hiyo kesho nitaiita leo. Alafu wewe ikifika hiyo kesho utaniambia subiri kesho tena. Mimi sio mtoto, sio mjinga.
Kesho inakuja na mambo yake, nani alijua mwaka huu ungevurugika kwa Corona, nani alijua? Alafu unambie habari za kesho, sijui mwakani wakati wewe unakula bata, hiyo haipo kwangu.
Mimi sio wale wa Kesho ya Manyani. Wewe tangu 1961 Nchi inapata uhuru kesho haifiki tuu, kesho gani hiyo. Tangu 1961 huko kabla hata mama na Baba yangu hawajazaliwa, Wanakuja kuzaliwa wanaambiwa subiri kesho, tunajenga mazingira, hahahahah! Mazingiraaa! Mazingira mpaka leo wameota mvi mazingira yanajengwa. Hahahah!
Mliwadanganya wazazi wangu lakini mimi hamtanidanganya ng'ooo!
Magufuli mimi sitakuchagua, ahadi za kesho mimi zisitaki kwani najua ni uongo. Wewe kesho huijui na hakuna aijuaye. Siku zote kesho ni yamanyani, leo ni leo, leo ndio yetu.
Watakuchagua hao hao ambao tangu 1961 wanaisubiri kesho waliyoahidiwa. Mpaka wamezeeka, wengi wamejifia kwa ufukara na fedheha wakiisubiri hiyo kesho huko makaburini. Sasa watoto wao na wajukuu wao nao wanaisubiri kesho ya kufurahi, kuneemeka, kucheka, kula bata. Nao watazeeka na kujifia katika umasikini uliotukuka wakisubiri kesho isiyofika.
Wewe Tangu 1961 kesho haijafika, alafu anakuja mtu anakuambia anataka kukuonyesha maajabu ndani ya miaka mitano mingine ukimchagua, ilhali umempa miaka mitano hakuna alichokufanyia wewe binafsi, zaidi ameminya waliokuwa kwenye mfumo na kuwabana walionje ya mfumo hataki kuwaajiri, ati ataajiri kesho. Hahahah!
Magufuli unataka nikuajiri kwa kukupa Kura ili uwe Rais alafu wewe hutaki kuniajiri, Looh! Hivi inakuja kweli hata kama ningekuwa kichaa wa kiwango gani bado nisingeshindwa kujua kuwa umenidharau. Wewe ule bata mimi nisote. Wewe upulizwe na kiyoyozi ofisini alafu mimi nipulizwe na vumbi mtaani nikisaka pesa madafu. Wewe utembee na misafara ya magari ya gharama ikikusindikiza kwa mbwembwe alafu mimi nichakaze soli za viatu nikiuza karanga baada ya kutembeza bahasha miaka nenda rudi. Magufuli, mimi sio chizi, sitakuchagua hata ulie.
Uzuri ni kuwa, mimi ninakura moja, hivyo haitakusaidia chochote. Sitapunguza wala kuongeza kwenye ushindi wako.
Watakuchagua hao wanaosubiri kesho ya tangu 1961, iliyowazeesha wazee wao kwa umasikini na ufukara.
Watakuchagua hao watakaokubali wakuajiri ili wewe usiwaajiri. Yaani wakupe ulaji alafu wewe uwanyime ulaji. Ili wateseke na kumenyeka mtaani wakati wewe ukila bata na kulindwa kwa ulinzi mkali.
Watakuchagua hao uliowaambia ukweli kuwa hutawaongezea mishahara yao kwani unajenga nchi kwanza ili kesho yao iwaneemeshe, nao wakachekelea wasijue nchi hii kesho ilianzwa kutafutwa tangu 1961 mpaka leo bado haijapatikana, ati wewe miaka mitano iliyobaki ndio uilete kesho yenye kicheko. Hao ndio watakuchagua.
Kesho ni yamanyani. Mimi natumia kanuni ya nipe nikupe. Hao wanaotumia kanuni ya nikupe alafu uwaambie kesho nitakupa ndio watakuchagua.
Magufuli sitakuchagua hata kama utaumia kusikia hivi, huo ndio ukweli.
Unidanganye mimi kama demu au mtoto mdogo. Hata Mademu wa siku hizi wanaakili. Hawadanganywi kienyeji. Yaani Demu anahitaji pesa alafu unamjia na maneno matupu ya ahadi hewa. Mademu wa siku hizi wanajua ahadi wapewazo na wanaume ndizo hizo walizopewa mama zao enzi hizo. Mpaka wa leo mama zao ni masikini na fukara wa kutisha. Leo demu umpe maneno matupu, sijui kesho Mungu atasaidia, nani anataka ya kesho bhana! Tupo leo, Maisha ni leo.
Magufuli sitakuchagua hata ukasirike
Magufuli sitokupa kura yangu hata ulie
Tunga vya kutunga lakini kura yangu hutopata.
Cheza Singeli, sijui amaboko, hata ukimaliza na mapanga shwaa! Hutopata kura yangu.
Taikon nimemaliza, huo ndio ukweli, unafiki hakuna hapo. Wewe utaki nile alafu unataka nikupe kula? Hahahaha! Wasubiri wazee wa kesho ya Manyani.
Hata Ukipita jua kabisa sikukupa kura, wala sitasema uongo na kujipendekeza kuwa nilikupa, nikikuchekea chekea kwa unafiki. Kura yangu hutapata kama Mungu aishivyo.
Leo sitaki maswali. Kama utampigia kura mpigie, kama hutompigia utajua mwenyewe. Ila msimamo wangu upo hivyo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300