Magumu Yasikutishe

Magumu Yasikutishe

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

MAGUMU YASIKUTISHE

Wengi wanaacha kutimiza malengo mara magumu yanapotokea lakini magumu ni kichocheo cha kuinoa akili yako kutenda katika viwango vya juu vya ubora lakini zaidi hukusaidia kuwa imara na usiyetetereka huko katika ufalme wa mafanikio yako. Leo nitakupa mfano wa wazi. Watoto wa maskini wengi hufaulu vizuri huko mashuleni kwa kuwa umaskini unawakera na wanaona elimu ni njia ya ukombozi lakini watoto wengi wa matajiri hawafanyi vizuri huko mashuleni si kwa kuwa hawana akili bali hawana jambo linalowasukuma kusoma kwa bidii.

Wahindi wengi (niliopata kusoma nao) hawafanyi vizuri shuleni na wengne huishia njiani kwa kuwa hawana changamoto ya kuhitaji elimu ile ya darasani ila wanafanya vizuri katika maduka ya wazazi wao kwa kuwa kwao kufeli biashara ni kujiandaa kufa maskini. Kitu cha kujifunza ni kwamba, Pasipo changamoto ni nadra kwa watu kukubali kujituma. Hakuna anayetafuta ukombozi kama tayari ana ukombozi, hakuna anayetafuta uponyaji kama ni mzima, hakuna anayetafuta shibe kama amevimbiwa. Hata kama umefanikiwa unaweza kujipa changamoto kwa kujiwekea malengo makubwa ambayo hata wewe yatakutisha maana kitisho ni changamoto.

Maisha yetu yamejaa changamoto nyingi sana hebu chagua changamoto za kuzipa kipaumbele na uanze kuelekea kufanikiwa kutokana na msukumo wa changamoto hizo. Kila changamoto ina msukumo wake na majibu yake. Changamoto ya usafiri husukuma juhudi za kutafuta baiskeli, pikipiki au gari na zaidi, kwa hiyo hapo itategemea na uzito uliouweka kwa changamoto uliyoipa kipaumbele, ila mtu hupokea anachokifikiria kichwani mwake na SI ZAIDI YA PALE.
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
Instagram Account: Elimu_biashara
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda sana hii kitu; umesema ukweli mtupu. Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa ukitaka mafanikio basi ondoka kwenye "comfort zone". Akatoa mfano wa mfanyakazi alieajiriwa, analipwa kidogo, ana manyanyaso mengi, amekopa ananuka madeni ila kila wazo analolijaribu au kuliwaza anashindwa na kujifariji kuwa mwisho wa mwezi atapata salary!

Mwingine akasema hivi; kama umedhamiria basi utapata suluhisho kwa kila changamoto lakini kama huna dhamira ya dhati basi utapata changamoto kwa kila suluhisho!
 
Biashara hasa professional buz zina changamoto zake ' ufahamike kwanza nk
 
Back
Top Bottom