Magwanda ya CHADEMA yaundiwa zengwe UDOM

Magwanda ya CHADEMA yaundiwa zengwe UDOM

NGOWILE

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
454
Reaction score
258
Uongozi wa chuo kikuu cha dodoma unaandaa mkakati wa kukataza wanafunzi kuvaa vazi la kichadema(gwanda) kwa kile wanachokiita kupiga vita siasa chuoni.hii imetokana na asilimia kubwa ya wanafunzi kuonekana kuwa wanavaa gwanda pamoja na skafu zenye rangi za chadema kana kwamba ndio sare ya chuo kwa hivi sasa. Habari hizi nimezipata kutoka kwa mwanachadema mmoja ambae anafanya kazi ofisi ya deputy vice chanselor(pfa) na hakutaka nimtaje jina lake. Chakujiuliza ni kwanini unapoingia chuoni kupitia chimwaga kuna bango lenye maandishi ccm?
 
Hiyo ndo kazi wanayoiweza hao wazee. wameshindwa kuwalipa walimu wetu mishahara yao mipya tangu wawapromote mwaka jana november 26, 2010. Nadhani na hujiuliza hivi mh Rais hawa wazee watatu (VC, DVC-ARC na PFA) uliwateua waje kutesa watanzania hapa udom? kama sivyo mbona wanajidai kuwa wana mtu huwa anawakumbatia na wewe mh Rais unatajwa? Kama huwakumbatii ama hawakumbatiwi na serikali yako kazi yao ilikuwa kujenga magorofa na sio kuwa daraja kati yao na serikali kuwezesha wafanyakazi na wanafunzi kupata haki zao?

Hivi kweli waheshimiwa Mkulo, Ghasia na Kawambwa mmekubali kabisa walimu hawa kulipwa mishahara isiyostahili yao kwa mwaka sasa wakati wenzao SUA, MUCE, DUCE na UDSM wakishakuwa promoted mwezi unaofuatia wanalipwa stahili zao?, Hawa wa UDOM wana hazina yao peke yao ambayo pia iko nje ya nchi hii?

Najiuliza huyu pfa, mhasibu mkuu na director human resource wangekuwa wanafanya kazi china wangekuwa bado hai kweli kwa ukatili, dharau na kutokuwajibika kwao huku?
 
kwani ni kosa la jinai mtu au watu kuamua kuvaa nguo zenye rangi ya kaki? ndio maana sasa wameamua kuwabadilishia migambo sasa wanavaa kijani. na wao wawatafutie sare nyingine. kufanya hivyo ndio wanawapa vijana wapambanaji ujasiri zaidi wa kuichukia ccm. wafanye wafanyavyo ila wajue ccm they are days are numbered.
 
Bora wapige marufuku hayo Magwanda, wamekwenda kusoma au kuvaa magwanda kama kuna wanafunzi wanataka kuvaa Magwanda wasubiri wamalize chuo
 
Bora wapige marufuku hayo Magwanda, wamekwenda kusoma au kuvaa magwanda kama kuna wanafunzi wanataka kuvaa Magwanda wasubiri wamalize chuo

Wangapi wanavaa nguo za magamba pale na hatujasikia wakikatza? Usiongee usilolijua
 
kilichopo ni wana vyuo vyote TANZANIA tuungane kudai haki yetu KIKATIBA kwani katiba inasema kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa akishatimiza miaka kumi na nane hili la wizara na vyuo halikubariki mbele ya sheria
 
Wangapi wanavaa nguo za magamba pale na hatujasikia wakikatza? Usiongee usilolijua

Haya wewe unaolijua endelea kuvaa hayo Magwanda tuone kama hao CDM watakusaidia chochote zaidi ya kukupa pole na kuitwa mpambanaji
 
CDM iko kwenye mioyo ya walio wengi. Wenyewe wanakereka na nini watu kuwa ktk upande waupendao au wanataka kuona wamevaa magamba? Magamba sasa wamefilisika hata upeo wa kusoma alama za nyakati au ndo mmepigwa upofu?
 
msichanganye siasa na elimu, fuata kilichokupeleka tusua GPA yako ya ukwel, uone utam wa maisha. Ushabik usio na msing utakufukuzisha chuo na hutamuona mwanasiasa hata mmoja aje kukutetea. Tanzania hamna siasa kuna mfumo wa kuchumia tumbo.
!!Changanya na zako!!
 
''ah! Wewe umenizidi tu kwa urefu umaskini na ujinga. . . . . Ila mimi nimekuzidi kwa pesa, elimu, wanawake, watoto . . . . Embu toka hapa, tulio ajiriwa UDOM Ni wa3 bwana, hao wengine ni dhiki zao zimewaleta'' Hayo co maneno yangu bali ni ya PFA ambayo alimtamkia m1 ya viongozi wa UDOSO
 
hii ni yao ni kali, wataanza kamata kamata mpaka mitaani sasa...
 
hiyo ndo kazi wanayoiweza hao wazee. Wameshindwa kuwalipa walimu wetu mishahara yao mipya tangu wawapromote mwaka jana november 26, 2010. Nadhani na hujiuliza hivi mh rais hawa wazee watatu (vc, dvc-arc na pfa) uliwateua waje kutesa watanzania hapa udom? Kama sivyo mbona wanajidai kuwa wana mtu huwa anawakumbatia na wewe mh rais unatajwa? Kama huwakumbatii ama hawakumbatiwi na serikali yako kazi yao ilikuwa kujenga magorofa na sio kuwa daraja kati yao na serikali kuwezesha wafanyakazi na wanafunzi kupata haki zao?

Hivi kweli waheshimiwa mkulo, ghasia na kawambwa mmekubali kabisa walimu hawa kulipwa mishahara isiyostahili yao kwa mwaka sasa wakati wenzao sua, muce, duce na udsm wakishakuwa promoted mwezi unaofuatia wanalipwa stahili zao?, hawa wa udom wana hazina yao peke yao ambayo pia iko nje ya nchi hii?

Najiuliza huyu pfa, mhasibu mkuu na director human resource wangekuwa wanafanya kazi china wangekuwa bado hai kweli kwa ukatili, dharau na kutokuwajibika kwao huku?

katiba mpya tuitakayo, itaje pia kiongozi asiyewajibika, adhabu kali dhidi yake na hasa kunyongwa kwa manufaa ya umma iwe kama uchina tu
 
Back
Top Bottom