Mahad Nur: Msomalia Wa City Mall na Victoria Plaza, Vijana wa Kitanzania tuko wapi?

Siri ya utajili wake anao yeye mwenyewe wewe lala amka kimbia huwezi jua na hawezi kusema hata kwa bunduki hayo mengine ni maneno ya vijiweni
 
Time time.Je wewe masaa 24 yako unayatumia vipi?.na wao.wanayatumia vipi?

Chunguza unavyo tumia masaa yako 24.

Make masaa kila mtu alipewa sawa yaani Hapo hakuna upendeleo. Sasa gap inaanzia kwenye kuyatumia hayo masaa 24
Hakuna lolote
 
Lakini tuongee ukweli, unamiliki kampuni inayoingiza mamilioni ya pesa mfano tuseme million 100, utaishi kwa kutegemea mshahara wa milioni 2?
Hapana, sema wanafanya mishe ela ya kampuni inachotwa vizuri tu, manunuzi hewa yanafanyika, usitegemee kukuta mmiliki na mkurugenzi waishi kwa mshahara
 
Mkuu bora umelichukua kama somo. Mimi mwenyewe nimejifunza sana sisi weusi kupeana support kwenye biashara ni ngumu.
 
Harusi ya 10M ndiyo inakufanya umkadirie mtu kiasi hicho? 10M kwa harusi za kitanzania mbona kidogo sana. Kama unakaa na mindset ya kutegemea misaada kiasi hiki utangoja sana ndugu yangu. Wakinga wanasaidiana kwa stile moja tu, Fanya kazi zalisha miaka yako itatimia UTATOLEWA (utapewa mtaji). Wahindi akija bongo anahustle kupata "mtaji", anapiga kazi kwa wenzake anatengeneza network, anajenga uaminifu, anapata mtaji ambao ni pesa ya kulipia pango la ofisi au godown tu...baada ya hapo mzigo atapewa na wadau. Fanya kazi acha kutegemea ndugu.
 
Sijui kama unaelewa hata maana ya sentesi sio chini ya, anyway kiufupi ni kwamba msaada ninao uhitaji mimi uko ndani ya uwezo wake kwa 100%. Mimi sihitaji kufungua kiwanda, ninahitaji starting point tu sijui unanielewa?! Msingi pekee ndio ninaoutafuta na wenyewe hauhitaji gunia la hela.

Pia naomba ufahamu kuwa mpaka nafikia hatua ya kwenda kuomba msaada kwake, nilikuwa tayari nimeshafanya jitihada kadhaa za kwangu mimi mwenyewe ikiwa ni pamoja na kutafuta wanafunzi wa kufundisha masomo ninayoyajua lakini bado nikakwama. Kwa hiyo sikukurupuka tu na kwenda kuomba handouts kwake.

Umeongelea wahindi na wakinga wanavyosaidiana, hapo kwa wahindi nakataa umetupiga kamba, kwa wakinga huko sijui. Wahindi wanatoka huko kwao wakifika hapa bongo hawana hustling ngumu ya kiivyo, wakifikaga hapa wamatukana na wahindi wenzao kwenye maduka au makampuni wanapewa kazi nzuri zenye malipo mazuri kiasi kwamba itakuwa ni rahisi kwao kutimiza lengo LA kupata mtaji kwa muda mfupi, Nina sema hivi sababu nina watu kibao tu wanafanya kazi NYANZA ROAD CO. na kila mwaka huwa wanakuja wahindi hawajui chochote wanakuwa juu yao huku wakilipwa mishaara mizuri kuliko hata wabongo wenye uzoefu wa siku nyingi. Kingine kubali kataa hakuna watu wanaokopeshana kama wahindi hakuna, nenda hata kwenye benki zao fualtilia uone mashariti raisi waliokewa. Kuhusu wahindi usitufanganye kabisaa.

Nakubaliana na wewe nijifunze kujitegemea hata katika hali ngumu vipi sababu ndio jamii yetu ilivyo kila mtu chake. Na pia mimi sio mvivu isipokuwa mazingira tu ndio yanayokutegenezea hiyo taswira kuhusu mimi. N ingekuwa mvivu sidhani kama hata ningekuwa nimeumiza kichwa na kudesigne project ya kufanya.
 
Alafu unaonekana una hela sana, naomba ajira mkuu.
 
Mkuu bora umelichukua kama somo. Mimi mwenyewe nimejifunza sana sisi weusi kupeana support kwenye biashara ni ngumu.
Mkuu yatupasa tuondoe kabisa haya mawazo na tukomae sisi wenyewe tu hata kwa udalali kama na wewe hali unayokutana nayo huko ni kama yangu. Sisi weusi yetu majivuni na ubinafsi, ushirikiano wetu ni kwenye misiba tu.

Kuna madogo wa kiarabu nilimaliza nao Form four miaka almost kumi iliyopita, wao walifeli hawakwenda advance, nadhani unazifahamu vizuri familia za kiarabu zilivyokuwa na strong unity. Leo ukikutana na hao madogo wanatembelea Prado na tayari wana familia zao, sometimes hata kupiga nao stori huwezi.
 

Duh! Huwa sipendi "kubishana", huwa napenda kujadiliana! Wahindi wanaokuja na kufikia kupata kazi zenye mishahara mizuri ni wachache sana, wengi wanaishia kufanya kazi store tu na kulipwa laki 5 mpaka 8 kwa mwezi, wabongo wanaona wanalipwa nyingi kwa sababu katika position hiyohiyo utakuwa mtanzania analipwa 250-3500 ndiyo maana wanalalama, lakini mwisho wa siku zote ni pesa ndogo hata ukigeuza mhindi umpe laki2 mbongo umpe laki 8 bado baada ya miaka 5 mhindi atakuwa na biashara yake na mbongo bado atakuwa anafanya kazi palepale! Hebu peleleza wahindi wengi waliotoka jinsi walivokuja, ninao rafiki wengi sana wa kihindi ndugu, wengine maisha yaliwabana mpaka wakaomba hifadhi kwa waswahili!!!!!! Anyway tuachane na hayo. Hebu nikuulize swali, huyo kaka yako alipewa mtaji nanani?!!....Kwanini unahisi kwamba una haki sana ya kupewa pesa na yeye?
 
Wala hata sio kubiashana, nilikuwa nakurekebisha tu hapo ulipo danganya hili kujustify unachokiamini, bado nakukatalia kabisa kwenye suala la kupata starting points wahindi huwezi ukawalinganisha na mbongo wao wana privileges. Mbali na kusaidiwa kazi yenye maslahi ya kiupendeleo unafahamu mashariti rahisi yaliyopo kwenye hizi benki zao ambazo ziko diaspora chini ya diaspora community OCI(Oversees Citizen of India)? Wewe unafikiri huwa wanaambiwa eti kupata mkopo ni hadi awe na nyumba pamoja na biashara ya miaka miwili??? Muhindi ana privileges wewe sema hapo kwenye nidhamu ukilinganisha na mbongo nnakukubalia.

Kuhusu huyo kaka yangu hakupewa mtaji wowote kwanini yeye alimaliza tu masomo ya juu akapata ajira miezi michache baadae! Ni kipindi ambacho tatizo la ajira lilikuwa bado halijawa sugu kama ilivyo sasa hivi. Binafsi naona Nina haki ya kusaidiwa na yeye sababu ni mwana ukoo mwenzangu na Niko kwenye hali ambayo inahitaji msaada. Na ninaamini endapo kama atanisaidia atakuwa amenisaidia sio tu mimi bali ukoo mzima kwa ujumla wakiwemo watoto wake.

Inaonekana wewe ni muhumini mzuri wa mfumo wa maisha ya kibepari. Hilo linawezekana palipo na msingi mzuri na mazingira ya nchi nzima kwa ujumla sio kwa Tanzania hii ambayo juzi hii nimeskia kati ya 100 ni watu 8 tu ndio wana uwezo wa kujitegemea. Na pia unemployment inatisha sana wala hakuna mipango thabiti ya kukabiliana nayo zaidi ya kejeri tu za wana siasa kuwaita wanainchi wao wavivu
 
Wewe umefikia wapi ndugu?
 
Tatizo mtaji, au unadhani hao walikuja bongo hawana hata 100 mfukoni......mbona wapo watanzania wamefanikiwa nchi za watu huko lakini walikua na mitaji.....na ujue mitaji inakua na siri nyingi nyuma ya pazia, wengine wamerithi, wamepewa na wazazi, wameua, wamehongwa, wameiba, wamedhurumu....

So live your usiige kuwa mbona mgeni kafanikiwa na wewe lazima ufanikiwe...
 
Wasomali ni wapambanaji sana,iwe kihalalai au kwa magumashi.nina marafiki wengi wakisomali,wanawake ni majasiri kuliko hata wanaume wa kibongo.
Inamaana wewe ukienda somalia unakua sawa na mwanamke hahahaha
 
ishu za kisomali achana nazo kabisa........wapo kama utando wa buibui.....huwawezi......
 
Mshahara 2m(mfano)
Ada ya shule ya watoto wote (private) kampuni inalipa
Kodi ya nyumba
Mafuta ya gari
Etc

Hivyo vyote unajilipia kwanza.
 

Toa ushauri wako mkuu wafanye nini na wao wapate hizo hela kama wawekezaji wa kisomali sio uwatolee povu tu
 
Nnaona vijana wanajibu hoja nzito kwa majibu mepes sanaaa, kama wasomali wanateka meli nanyie mkateke kwan si mna bahari? Vijana tupambane tuache visingizio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…