DOKEZO Mahakama chunguzeni rushwa mahakama ya mwanzo Arusha(Maromboso)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Posts
9,213
Reaction score
14,925
Ni muda sasa nimekuwa nahudhuria kusikiliza kesi za ndugu/marafiki katika mahakama hii ya mwanzo Arusha maarufu kama Mahakama ya Maromboso, hasa kesi zinazo sikilizwa na mfawidhi wa hii mahakama (sito taja jina)

Huyu bwana hata kama haki iko upande wako, usipo toa rushwa hakuna jinsi utashinda hiyo kesi.

Cha kufurahisha ukikata rufaa kutokuridhika na maamuzi ya huyu mfawidhi una shinda rufaa.

Najiuliza kwanini walioko juu yake hawajiulizi kwanini iwe hivyo? Kwanini asishushiwe madaraka au kupewa adhabu za kinidhamu?

Watu tuna poteza haki zetu kwa sababu ya rushwa. Haki haionekani ikitendeka Maromboso
 
Ala kwa urefu wa kamba yake YAKHE!
 
Kwani ww umewahi kuckia mkuu wao akikalipia rushwa kwa kumanisha kutoka rohoni?.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Ni muda sasa nimekuwa nahudhuria kusikiliza kesi za ndugu/marafiki katika mahakama hii ya mwanzo Arusha maarufu kama Mahakama ya Maromboso, hasa kesi zinazo sikilizwa na mfawidhi wa hii mahakama (sito taja jina)

Huyu bwana hata kama haki iko upande wako, usipo toa rushwa hakuna jinsi utashinda hiyo kesi.

Cha kufurahisha ukikata rufaa kutokuridhika na maamuzi ya huyu mfawidhi una shinda rufaa.

Najiuliza kwanini walioko juu yake hawajiulizi kwanini iwe hivyo? Kwanini asishushiwe madaraka au kupewa adhabu za kinidhamu?

Watu tuna poteza haki zetu kwa sababu ya rushwa. Haki haionekani ikitendeka Maromboso
Hivi kuna yule hakimu anaitwaga toto..Kuna wakati alikuwa na kesi za shangazi yangu mbili...za kumkomesha. Na alimkomesha shangazi yangu haswa...maromboso kwa rushwa ni hatari. Hivi Toto yupo? Toto alikuwa anakaa ofisi Moja na hakimu mwanamke mweupe mjema kama sikosei naomba nisahihishwe..kazi Yao kula rushwa za wakopeshaji mikopo umiza, wao wanatoa amri za kukamata Mali za wateja..na wale wakopeshaji hawana hata leseni...maromboso iliharibika sana sana. Wamrudishe yule James labda pataimarika
 
Back
Top Bottom