Hivi kuna yule hakimu anaitwaga toto..Kuna wakati alikuwa na kesi za shangazi yangu mbili...za kumkomesha. Na alimkomesha shangazi yangu haswa...maromboso kwa rushwa ni hatari. Hivi Toto yupo? Toto alikuwa anakaa ofisi Moja na hakimu mwanamke mweupe mjema kama sikosei naomba nisahihishwe..kazi Yao kula rushwa za wakopeshaji mikopo umiza, wao wanatoa amri za kukamata Mali za wateja..na wale wakopeshaji hawana hata leseni...maromboso iliharibika sana sana. Wamrudishe yule James labda pataimarikaNi muda sasa nimekuwa nahudhuria kusikiliza kesi za ndugu/marafiki katika mahakama hii ya mwanzo Arusha maarufu kama Mahakama ya Maromboso, hasa kesi zinazo sikilizwa na mfawidhi wa hii mahakama (sito taja jina)
Huyu bwana hata kama haki iko upande wako, usipo toa rushwa hakuna jinsi utashinda hiyo kesi.
Cha kufurahisha ukikata rufaa kutokuridhika na maamuzi ya huyu mfawidhi una shinda rufaa.
Najiuliza kwanini walioko juu yake hawajiulizi kwanini iwe hivyo? Kwanini asishushiwe madaraka au kupewa adhabu za kinidhamu?
Watu tuna poteza haki zetu kwa sababu ya rushwa. Haki haionekani ikitendeka Maromboso
Ni muda sasa nimekuwa nahudhuria kusikiliza kesi za ndugu/marafiki katika mahakama hii ya mwanzo Arusha maarufu kama Mahakama ya Maromboso, hasa kesi zinazo sikilizwa na mfawidhi wa hii mahakama (sito taja jina)