Mahakama Kenya yazuia usajili wa vidole

Mahakama Kenya yazuia usajili wa vidole

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563

Mahakama Kuu Kenya imesitisha kutekelezwa kwa mfumo wa usajili wa wananchi kwa njia ya alama za vidole hadi hapo sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa.

Mbali na kuzuia utekelezaji huo, mahakama imesema kuwa kukusanya taarifa za eneo (GPS) na vinasaba (DNA) ni kinyume na katiba ya nchi.

Serikali ya Kenya imekuwa ikikusanya taarifa mbalimbali katika usajili huo ikiwa ni pamoja na alama za vidole, taarifa za familia, na eneo kamili mtu analoishi.

Wakati wa zoezi hilo ambalo serikali ilisema ni la lazima wale wote ambao hawatojiandikisha hawatopata huduma za msingi za serikali kama vile pasi ya kusafiria (passport), na cheti cha kuzaliwa.

Mahakama imezuia zoezi hilo kwa kile ilichoeleza kwamba wananchi wanaweza kujikuta katika hatari isiyorekebishika endapo taarifa zilizokusanywa zitatumiwa vibaya.

Majaji watatu wa mahakama hiyo waliamuru kusitishwa kwa mpango huo unaofahamika kama Huduma Namba hadi sheria ya kina ya kulinda taarifa zinazotolewa na wananchi upitishwe.
 
Tanzanians are exposed
 
Nimeelewa kwanini madiplomat na wageni hawachukuliwi alama za vidole kwenye zoezi la usajili wa line za simu. Sheria za hizo nchi zao za kuhifadhi taarifa za mtu hasa biometric ngumu sana.

Kwetu kilichotuponza ni vyombo husika kutokufanya kazi na majukumu yao matokeo yake wamejikita kwenye kuunga juhudi.

Hongereni majirani zetu

MK254
 
LOL sasa sheria zao zina uhusiano upi ndani ya ardhi ya Tanzania? Acha kuongea pumba, ukishaingia Rwanda hauna cha excuse kwamba sifuati sheria za Rwanda kisa mimi ni mtanzania, zipo immune system za diplomats lakini hazina uhusiano vile vile na sheria zote.

Kwa taarifa yako tu TCRA inawaandalia utaratibu wao kwa kupitia credentials zao na wao watahitaji kujisajili kwa alama za vidole.
 
Excellence. Check and balance, kila chombo kifanye kazi yake... sio kama kwa akina Adela; Chombo kimoja kikifanya maamuzi huruhusiwi kupinga; ukipinga unapewa kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na elfu thelathini isiyo na maelezo. 😁 😁
 
LOL sasa sheria zao zina uhusiano upi ndani ya ardhi ya Tanzania? Acha kuongea pumba, ukishaingia Rwanda hauna cha excuse kwamba sifuati sheria za Rwanda kisa mimi ni mtanzania, zipo immune system za diplomats lakini hazina uhusiano vile vile na sheria zote.

Kwa taarifa yako tu TCRA inawaandalia utaratibu wao kwa kupitia credentials zao na wao watahitaji kujisajili kwa alama za vidole.
Hizo alama za vidole mnataka kuzifanyia nini ninyi wakolomije?

Mbona mmezing'ang'ania sana?

Mnataka kwenda kutambika nazo chattle?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imagije Nida wana hadi namba ya nyumna ninayoishi.
Hilo sio Tatizo, tatizo ni kuwa hawana utaalamu wa kuzuia hizo data zisiibiwe.
Kama tu watu wakiwa wengi mtandao wao unafeli unadhani wana technology ya ku protects privacy zetu?

Hawana!
Nida wapo kizamani sana fikiria website yao inatumia aspire net kwenye back end enzi hizi za node.js
 
LOL sasa sheria zao zina uhusiano upi ndani ya ardhi ya Tanzania? Acha kuongea pumba, ukishaingia Rwanda hauna cha excuse kwamba sifuati sheria za Rwanda kisa mimi ni mtanzania, zipo immune system za diplomats lakini hazina uhusiano vile vile na sheria zote.

Kwa taarifa yako tu TCRA inawaandalia utaratibu wao kwa kupitia credentials zao na wao watahitaji kujisajili kwa alama za vidole.

Sawa mkubwa mie naongea pumba lakini najua nnachokisema na kukiandika. Wenzetu walioendelea taarifa za mtu binafsi ni kitu nyeti sana. Usijekuona kwenye website kuna privacy policy ukajua wanajiwekea tu, ni takwa na sheria iwe hivyo.

Kama wanaandaa utaratibu hadi hapo utakapokua tayari ndio kuchukua alama zao za vidole zitachukuliwa, kwa sasa zitatumika namba zao za Diplomat.

Jitahidi kuelewa mahusiano ya kidiplomasia na makubaliano ya kimataifa juu ya baadhi ya mambo.
 
Wameachwa kwa sasa sababu zoezi linahusu kitambulisho cha taifa ambacho obviously wao hawawezi kuwa navyo, lakini NIDA ikimalizana na wa Tanzania watawapa utaratibu deplomats na visitors Wote kupitia passports zao nao watawekewa utaratibu wa kusajili kwa kupitia fingerprint technology, haikwepeki hiyo

Hiyo ya sijui sharia zao hazicomply na zetu ni pumba ambayo unatakiwa uone aibu kuizungumza mbele za watu wazima.
 
You are right Sir!

IMG_20200203_152828_096.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20200203-152550.jpg
    Screenshot_20200203-152550.jpg
    101.2 KB · Views: 1
Wameachwa kwa sasa sababu zoezi linahusu kitambulisho cha taifa ambacho obviously wao hawawezi kuwa navyo, lakini NIDA ikimalizana na wa Tanzania watawapa utaratibu deplomats na visitors Wote kupitia passports zao nao watawekewa utaratibu wa kusajili kwa kupitia fingerprint technology, haikwepeki hiyo

Hiyo ya sijui sharia zao hazicomply na zetu ni pumba ambayo unatakiwa uone aibu kuizungumza mbele za watu wazima.
Hizo fingerprints mnataka kuzipeleka wapi?

Maana kimsingi, kwa uwezo wenu duni, hamna ujuzi wala maarifa ya kuzitumia fingerprints kwenye maswala ya ujasusi na intelijensia.

Uwezo wenu uko very limited. Ujasusi wenu ni wa kukimbizana na vibaka wanaomtukana magufuli.

Sasa najiuliza, hizo fingerprints mlizozikusanya mna shughuli gani nazo?

Ni ulimbukeni au kutoelewa dhima ya fingerprints?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom