Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Pamoja na ukweli kwamba Ibara ya 107A(2)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitaka Mahakama kutoa haki bila kujifunga na mambo ya kiufundi kiasi cha kushindwa kutoa haki,mambo kwa upande wa mahakama zetu ni tofauti kabisa hususan kwenye mashauri ambayo yanahusu kushitakiwa kwa serikali au vigogo wa serikali.
Kumekuwa na muendelezo wa kesi nyingi kushindwa kutolewa maauzi yenye tija kwa umma kwa kigezo tu cha kasoro za kiufundi ambazo ukizichunguza huwa hazina uzito ukilinganisha na uzito wa ile haki inayodaiwa.
Nimejaribu kufuatilia kwenye Kesi ya Ado Shaibu v.Honorable John Magufuli,Misc Civil Cause No.29 of 2018,kesi ambayo ilipinga uteuzi wa Adelarus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu kwa kuwa hakuwa na sifa.Badala Mahakama kujikita katika kutoa uamuzi wa hoja iliyopo mezani,iliamua kujikita katika kijadili mambo na mapungufu ya kiufundi katika kesi husika na kushindwa kutoa uamuzi wenye tija kwa taifa.
Nikiangalia hata katika kesi inayoendelea ya Pauline Gekul na Ndugu Hashim Ally,naona Mahakama imejikita kushughulikia mambo ya kiufundi katika kesi hiyo badala ya kujadili haki ya msingi ambayo ndugu Hashim Ally anaiomba Mahakama impatie.
Ni wazi kwamba mambo yote haya,yanasbabishwa na udhaifu wa mfumo wettu wa utoaji haki.Na ubovu huu unasababishwa na Mahakama yetu kutokuwa huru,kiasi cha kuingiliwa uhuru wake na mihimili mengine.
Ni wazi kwamba mahakama kujikita katika mambo ya kiufundi badala kusimamia utoaji wa haki katika malalamiko yanayowasilishwa hususan yanayohusu serikali ni ishara ya namna mahakama ilivyo na uoga kuiwajibisha serikali katika mashauri ya msingi.Hivyo njia pekee huwa ni kuchambua kasoro za kiufundi kama njia pekee ya kukwepa kuiwajibisha serikali
Kukosekana kwa uhuru huku ndio husababisha kupatikana kwa majaji na mahakimu wasiokuwa na sifa,ambao wameendelea kuwa mzigo kwa mahakama na taifa kwa ujumla.
Ni wazi kwamba kuna haja ya kufanya mageuzi ya haraka ili kuboresha mifumo yetu ya utoaji haki ili kulinda maslahi ya Taifa.Na njia pekee ya kuboresha mifumo hii ni kupata katiba mpya ambayo itasimamia mifumo na kuhakikisha mahakama zinakuwa huru