Mahakama zetu zimegawanywa kwa vitengo na mienendo tofauti tofauti kwa kuanzia chini kwenda juu, chini kwa maana ya mabaraza ya kata, wilaya, mahakama za mwanzo, wilaya, hakimu mkazi, kuu na Baba lao mahakama ya rufaa... sasa makosa mengi hasa ya kihalifu ni lazima yaanzie ngazi za chini kwanza ili kuweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji taarifa za awali, ushaidi, utambuzi wa waarifu, aina ya kosa mpaka kosa kua completed na kupelekwa mahakama husika, mfano kesi za mauaji itawalazimu kwanza kuanzia mahakama ya wilaya ili kukamilisha mambo yote haya nliyokutajia then kesi hio itapelekwa mahakama husika ambayo ni kuu, lengo vile vile ni kuokoa muda sio kumkimbizia mtu kwenye mahakama kubwa ilihali mahakama hio kwa namba iko ndogo na ina kesi nyingi za kuskiliza so wanatakiwa wakienda huko kila kitu kiwe kinajulikama then kesi ianze mara moja.
Sheria imekua tofauti kwa upande wa madai kwakua huku bwana wanaangalia thamani ya deni, mali au madai yenyewe na utaona sheria kama CPC inatamka wazi tu kua kama kutakua na madai ya kiasi flani basi mdai atalazimika kwenda moja kwa moja mahakama flani.