KESI IMEFIKA PATAMU, SASA DUNIA YOTE ILIYOKUWA HAIFAHAMU MATENDO YA CCM YA AWAMU YA 5 NA YA SASA YA AWAMU YA 6 YATAANIKWA NA KUFAHAMIKA KINAGA UBAGA
Kesi hii ya Mbowe itakuwa ktk vitabu kama kesi ya serikali ya makaburu dhidi ya Nelson Mandela. Kesi hii itasomwa ktk historia baada ya CCM kungolewa kutoka madarakani kwa kupitia uchaguzi huru kama kesi ya : Mpinzani Freeman Mbowe ndani ya 'mahakama' za CCM. ifahamike katika mabano neno 'mahakama' ni kuwa CCM inataka kuburuza Mahakama zitumike vibaya pamoja na mfumo wa kusimamia / kuchunguza za jinai (criminal justice system) nzima, lakini imani yetu bado ipo kuwa Mahakama hapa bila "mabano" ni mhimili huru na itatenda haki na kukataa mbinyo wa aina yoyote ile toka upande wowote.
Historia inasema makaburu waliokuwa ktk serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini iliona waAfrika raia wengine waliokuwa wanadai kuwa watu-uhuru, kutaka demokrasia shirikishi na Marndeleo ya watu wote walikuwa ni hatari na wangeweza kuchelewesha maendeleo ya vitu kama madaraja, reli, flyovers pamoja ni miradi mingine mikubwa iliyokuwa ya mfano barani Afrika. Madai hayo ya serikali ya kibaguzi ya wachache ya miaka hii yanarudiwa na CCM miaka hii ya 2015 - 2025. Na CCM pamoja na serikali yake kudai wapinzani ni watu hatari wasio na uzalendo na wasioitakia Tanzania maendeleo.
Soma utetezi wa Nelson Mandela alipofikishwa mbele ya korti na utetezi huo wa Nelson Mandela kuenziwa na watu wote duniani na taasisi kubwa za kimataifa na vyuo vikuu vijana kufunguliwa macho juu ya tawala kandamizi za kibaguzi, katili na vinazokandamiza utu wa watu na haki zao kwa kisingizio cha kujenga uchumi, madaraja, flyovers, mabwawa ya umeme n.k