Mahakama Kuu: Freeman Mbowe (CHADEMA) afungua shauri kupinga mashtaka dhidi yake

AMEN
 
6 August 2021
Dar es Salaam, Tanzania

MVUTO WA KESI YA MBOWE NA WENGINE 4 : WAENDESHA MASHTAKA WA SERIKALI WABADILISHA HATI YA MASHTAKA
Purukushani za media katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi Kisutu Dsm


Upande wa mashtaka leo siku ya ijumaa tarehe 6 Agosti 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu umebadilisha hati ya mashtaka yaliyokuwa yanamkabili mwenyekiti wa CHADEMA na wengine wanne.

Maoteo kuwa kesi inayomkabili kiongozi wa chama cha siasa cha CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake 4 kuvuta hisia mbalimbali za waandishi wa habari za media zote leo jijini Dar es Salaam Tanzania zimetimia.

Waandishi wengi wa vyombo vya habari walijitokeza ili waweze kuhabarisha umma wa waTanzania na dunia kwa ujumla na kila mwandishi habari alijitahidi kuhakikisha anaondoka na habari timilifu za picha za mnato, video, mitandao ya kijamii, magazeti, redio na Televisheni.

Tutegemee hali hii ya utulivu mahakamani ya waandishi kuweza kupata habari itaendelea namna hii mpaka hitimisho la kesi hii inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA kamanda Freeman Aikael Mbowe na wenzake 4.
Source : DARMPYA TV
 
jamani watanzania wenzangu wenye magonjwa kama;
1. KISUKARI
2. UKIMWI
3. SARATANI
4. KIFUA KIKUU
5. CELI MUNDU
Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu lina puputisha balaa, aise.
 
7 August 2021

PROF: LIPUMBA AMZUNGUMZIA MBOWE KUHUSU SUALA LA UGAIDI.



Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020. Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe anahoji Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.


Source : StarTV Habari
 

Haiishi hadi inapokwisha.

Aluta Continua.
 
jamani watanzania wenzangu wenye magonjwa kama;
1. KISUKARI
2. UKIMWI
3. SARATANI
4. KIFUA KIKUU
5. CELI MUNDU
Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu lina puputisha balaa, aise.

Waambie hawa:



Kuhangaika na watanzania ni kutojitendea haki.

Habari ndiyo hiyo.
 

Aibu kubwa sana kwa serikali ya SSH.

Mbatia, Zitto na sasa Lipumba wametoa misimamo yao.

Asasi za dini, azaki, madhehebu, vyama vingine nk matamko yenu kwenye kadhia hii yaliyochelewa mno yanakuwa hayana maana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…