Mahakama Kuu imesitisha usikilizwaji wa shauri la kinidhamu linalomuhusu Wakili Boniface Mwabukusi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

​
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, imesitisha usikilizwaji wa shauri la kinidhamu lililofunguliwa dhidi ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, katika Kamati ya Maadili ya Mawakili. Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji linaloongozwa na Jaji Amir Mruma, likielekeza kuwa hatua za shauri hilo zisubiri uamuzi wa shauri la msingi la kikatiba linalohusiana na mamlaka na mfumo wa kisheria unaosimamia kamati hiyo.

Hatua hiyo inafuatia shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mwabukusi kupinga uhalali wa baadhi ya vipengele vya sheria vinavyosimamia Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, mahakama imeamua suala hilo la kikatiba lishughulikiwe kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa kinidhamu dhidi yake.
 
ok. :1Head:
 
19 October 2026

Senior counsel Mwaisa Mpale Mpoki akifafanua kesi ya kikatiba Na. 25918 ya Mwaka 2026 aliyofungua Boniface Mwabukusi kuhusu Kamati ya Maadili

View: https://m.youtube.com/watch?v=nf3qe259o-c

Uamuzi wa Mahakama Kuu (Oktoba 19, 2026): Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dodoma chini ya jopo la majaji watatu (Jaji Amir Mruma, S.H. Hassan, na Irene Musokwa) imetoa amri ya kusitisha kwa muda usikilizwaji wa shauri hilo la maadili.

Zuio hili linasubiri kusikilizwa kwa Kesi ya Kikatiba (Na. 25918 ya Mwaka 2026) iliyofunguliwa na Mwabukusi kupitia timu yake ya mawakili waandamizi.
 
Back
Top Bottom