Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mahakama kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar Es salaam inatarajiwa Mei 22, 2025 saa mbili asubuhi mbele ya Jaji Obadia Bwegoge anatarajiwa kusikiliza Waasisi wa chama cha siasa cha Independent People's Party (IPP), wamefungua shauri Mahakama Kuu dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushindwa kukipa usajili wa muda chama hicho kwa miaka miwili sasa.
Katika maombi hayo, waasisi hao, Vyonheaven Urima na Andrew Bomani wamemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kama mjibu maombi wa pili.
Waasisi hao wa IPP wanaiomba Mahakama iwape kibali cha kufungua maombi ili itoe maagizo kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania kukipa usajili wa muda chama hicho kipya cha siasa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Waasisi hao wanalalamika kuwa Mei 3, 2023 waliwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, maombi ya kusajiliwa chama cha IPP kwa kujaza fomu kama inavyoelekezwa katika sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini.
Baada ya kuwasilisha maombi, wanadai Juni 8, 2023 Ofisi ya Msajili iliwaandikia barua yenye ikikiri kupokea maombi yao kwa ajili ya usajili wa muda wa chama hicho.
Katika barua hiyo, Msajili aliwataka wawasilishe nakala tete (soft copies) ya katiba ya chama, uthibitisho wa uraia wa waombaji, bendera ya chama, vyeti vya kuzaliwa vya waasisi hao na uthibitisho kuwa wamelipa ada ya usajili wa chama cha siasa.
Baada ya kupokea barua hiyo, waasisi hao walitimiza maelekezo na kuwasilisha nyaraka hizo kama walivyoelekezwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, wakiamini wametimiza matakwa ya kisheria kupata usajili wa muda.
Waasisi hao wameiomba mahakama iwape kibali wafungue maombi ya kisheria ili kuiagiza Ofisi ya Msajili kukipa usajili wa muda chama hicho.
“Labda tu kama maombi haya yatakubaliwa lakini tofauti na hivyo, waombaji wataathirika na kupata hasara isiyoweza kufidiwa kulinganisha na hasara ambayo wajibu maombi ambao ni Msajili wa vyama na AG wataipata,” wanadai katika hati ya kiapo.
Wanadai Msajili amekiuka vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019 ambavyo vimeweka masharti ya usajili wa chama cha siasa. Wanadai Msajili amewanyima haki yao ya kikatiba na amekaa kimya kwa miaka miwili.