Mahakama Kuu kusikiliza ombi la Kibatala kuhusu kutekwa kwa Polepole Oktoba 9

Mahakama Kuu kusikiliza ombi la Kibatala kuhusu kutekwa kwa Polepole Oktoba 9

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam imepanga Oktoba 9, 2025 kusikiliza maombi ya Wakili Peter Kibatala juu ya madai ya kutekwa kwa Mwanasiasa Humphrey Polepole.

Wakili Kibatala aliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura, Oktoba 7, 2025 akiiomba mahakama itoe amri ya Polepole afikishwe mahakamani ama mamlaka husika ziseme yupo wapi.

Kwa mujibu wa hati iliyosajiliwa baada ya kupokelewa kwa maombi hayo imepewa namba 24514 ya mwaka 2025 na imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi, ambapo katika maombi yake, Kibatala ameiomba Mahakama iingilie kati mara moja akidai kuwa Polepole alitekwa nyara alfajiri ya Jumatatu, Oktoba 6, 2025, kutoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam na watu wasiojulikana wanaoshukiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa Polepole hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai katika Mahakama yoyote, na kwamba kwa sasa inaaminika anashikiliwa katika eneo lisilojulikana na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Maombi hayo yamewasilishwa dhidi ya wajibu Maombi watano, akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RCO) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RPC).
1759912642619.png
 
Unavyo-copy Na kupaste n Kwamba sisi wengine hatuwezi kusoma ikiwa kwa mtoa mada au ndo kujitia umuhimu kwenye mada za watu, em acha ufala.
 
Sitaki kuamini kama Kibatala ni mjinga, huyu kuna kitu atakuwa anakijua na ushahidi anao.
Shita kila tunayemuona smart anagalagazwa chali asubuhi peupe alafu ndio tunagundua kumbe ni risasi ya maji. Anaibuka mwingine na matumaini hewa. britanicca
 
Unavyo-copy Na kupaste n Kwamba sisi wengine hatuwezi kusoma ikiwa kwa mtoa mada au ndo kujitia umuhimu kwenye mada za watu, em acha ufala.
Una makasiriko kama una mimba vile.
 
Huyo c mumeo lazima uje umtetee
Hunaga hoja, wewe na hananja au mabwana zako wa CCM. Hujui maana ya ku - emphasize? Ku-quote sehemu ya mada, ku -bold au ku- italicize ni kuonesha msisitizo au shule ulienda kusomea ujinga na uchawa.?
 
Matusi haya niya nini mkuu? mbona sioni hoja hapa kama taifa tuna mambo mengi yakuzungumza
Mm nampokea mtu kama alivyokuja, ngoja na mm niangushe makombora yangu, hakuna kukaa kinyonge.

Ameshobokea comment isiyomhusu, amefikia Hadi kunitukana na mm siwezi kukaa kinyonge.
 
Hunaga hoja, wewe na hananja au mabwana zako wa CCM. Hujui maana ya ku - emphasize? Ku-quote sehemu ya mada, ku -bold au ku- italicize ni kuonesha msisitizo au shule ulienda kusomea ujinga na uchawa.?
Kwahy huyo mumeo aki-emphasize Ndo unazingatia Ila Mtoa mada aki-emphasize huwezi kuzingatia?
 
Back
Top Bottom