Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Tarehe 16 Julai 2025, Mahakama Kuu ya Malawi ilitoa uamuzi wa kutangaza kuwa Kifungu cha 200 cha Kanuni ya Adhabu, kinachohalalisha kashfa kuwa kosa la jinai, ni kinyume na Katiba. Mleta maombi, Joshua Chisa Mbele, alipinga kifungu hicho akisema kinakiuka haki yake ya uhuru wa kujieleza inayolindwa na Kifungu cha 35 cha Katiba, na hakilingani na wajibu wa Malawi chini ya sheria za haki za binadamu za kikanda na kimataifa.
Ikumbukwe Joshua Chisa Mbele alifungua kesi dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali akipinga uhalali wa Kifungu cha 200 cha Kanuni ya Adhabu ya Malawi. Kifungu hicho kilieleza kwamba mtu yeyote anayechapisha taarifa za kumkashifu mtu mwingine kwa njia yoyote, kwa nia ya kumshushia heshima, anakuwa ametenda kosa la jinai la "kashfa".
Mahakama ilikubaliana na hoja hiyo kwa kusema kuwa kufanya kashfa kuwa kosa la jinai ni kikwazo kikubwa na kisicho na uwiano kwa uhuru wa kujieleza na kunadumaza mijadala ya umma. Mahakama ilisistiza kuwa haki ya kujieleza ni msingi muhimu wa demokrasia ya kikatiba ya Malawi, hivyo vizuizi vyovyote lazima viwe vya kisheria, vya haki, na vya lazima katika jamii huru na ya kidemokrasia. Mahakama ilihitimisha kuwa kwa kuwa kuna njia za madai za kiraia katika kushughulikia kashfa, basi adhabu ya jinai haihitajiki na ni kali kupita kiasi.
Gilbert Khonyongwa, wakili wa mlalamikaji, alisema, “Huu ni ushindi mkubwa kwa uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu. Wanahabari na vyombo vya habari sasa wanaweza kuripoti habari muhimu bila hofu ya kushitakiwa kwa jinai.”
Wesley Mwafulirwa, naye wakili wa mlalamikaji, aliongeza kuwa, “Kuondoa kashfa kama kosa la jinai ni hatua muhimu kwa Malawi kuwa jamii iliyo wazi zaidi. Mahakama imethibitisha kuwa uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi isiyopaswa kudhibitiwa kwa adhabu ya jinai.”
Kituo cha Sheria Kusini mwa Afrika (SALC) kimepongeza uamuzi huo kikisema utaimarisha mijadala ya umma na kukuza mjadala wa wazi kuhusu masuala muhimu ya jamii kama vile ufisadi. Melusi Simelane, kiongozi wa masuala ya haki za kiraia SALC, alisema, “Kuondoa kashfa kama kosa la jinai ni muhimu sana kulinda uhuru wa kujieleza na kuwezesha wanahabari na watetezi wa haki za binadamu kuwawajibisha wenye mamlaka bila hofu ya kifungo. Sheria hizi mara nyingi huleta hofu na kusababisha watu kujicenzor.”
SALC imeitaka Bunge la Malawi kufuta rasmi Kifungu cha 200 cha Kanuni ya Adhabu na pia kupitia sheria nyingine zinazoweza kukinzana na haki za kikatiba na za binadamu.

=============For English Aundience============
On 16 July 2025, the High Court of Malawi delivered a landmark judgment in a Constitutional case, declaring Section 200 of the Penal Code, which criminalises defamation, unconstitutional. The claimant argued that the provision violated his right to freedom of expression, protected under Section 35 of the Constitution, and was incompatible with Malawi’s commitments under regional and international human rights law.
The Court found that criminalising defamation under Section 200 imposes a disproportionate restriction on freedom of expression and stifles public discourse. It underscored that the right to freedom of expression, enshrined in Section 35 of the Constitution, is a cornerstone of Malawi’s constitutional democracy. The Court emphasised that any limitation on this right must be lawful, reasonable, and necessary in an open and democratic society, in line with international human rights standards. It concluded that the availability of civil remedies for defamation renders criminal prosecution not only unnecessary but also disproportionate.
Moreover, Section 200 lacks adequate safeguards to prevent arbitrary or excessive interference with free speech and cannot be justified as necessary or proportionate. It has also affirmed that freedom of expression is a fundamental right essential to a healthy democracy and should not be limited by criminal sanctions.”The Southern Africa Litigation Centre (SALC) welcomed the decision, noting that decriminalising defamation will significantly enhance public discourse by enabling open and honest dialogue on critical societal issues.
This ruling aligns Malawi more closely with recommendations from the African Commission on Human and Peoples’ Rights and other international human rights standards, promoting a more open society where reputations are safeguarded without undermining press freedom.”SALC urges the Malawi Parliament to take immediate action to repeal Section 200 of the Penal Code. It further urges Parliament to review related laws and regulations to ensure they align with constitutional and human rights standards.