Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama kuu ya Tanzania imewakumbusha mawakili wote wanaohudhuria mashauri mahakamani kuzingatia na kuheshimu maelekezo ya chama cha wanasheria tanganyika (TLS) pamoja na maelekezo ya mahakama, kwa lengo la kuhakikisha mwenendo wa mashauri unafanyika kwa ufanisi, heshima na kwa kuzingatia misingi ya haki.
Kauli hiyo imetolewa kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 137 ya kanuni za maadili ya mawakili na ibara ya 30 (1) (2) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano waTanzania.
Soma: Dkt. Nshala: Mawakili kuzuiwa kutoa muhtasari kwa waandishi ndani ya viunga vya mahakama si sawa, TLS ichukue hatua
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chama cha wanasheria tanganyika (TLS) kiliwataka wanachama wake kutoongea na vyombo vya habari katika maeneo ya mahakama mara baada ya mashauri kuahirishwa.
Mahakama kuu imeeleza kuwa, ili kurejea hatua hiyo ya chama cha wanasheria tanganyika na maelekezo ya mahakama ya Tanzania, inawakumbusha na kuwasisitiza mawakili wote wanaohudhuria mashauri mahakamani kuzingatia na kuheshimu maelekezo hayo.
Mahakama imesema hatua hiyo inalenga kuzuia mahusiano na vyombo vya habari katika viunga vya mahakama pamoja na kuzuia mazungumzo yanayoweza kuathiri mwenendo wa mashauri yanayoendelea mahakamani kwa namna inayoweza kuathiri mwenendo wa mashauri.
Aidha, mawakili wote wamekumbushwa kuwa, wawasiliane na mwenendo wao mbele ya mahakama na nje ya mahakama kuhusu mashauri yanayoendelea mahakamani kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yanayotolewa na mahakama zaTanzania.
Mahakama kuu imesisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha uendeshaji wa mashauri unafanyika kwa ufanisi, heshima na kwa kuzingatia misingi ya haki.
Taarifa hiyo imetolewa na msajili wa mahakama kuu ya Tanzania, C.M. Tengwa, tarehe 12 Agosti 2026.