Mahakama Kuu yaombwa kueleza kama ni halali kwa Mawakili wa TLS kuwatetea watuhumiwa waliombaka Binti wa Yombo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Shauri la maombi ya marejeo limefunguliwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma dhidi ya mawakili na washtakiwa katika kesi ya jinai ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.

Maombi ya marejeo namba 23476/2024 yamefunguliwa leo Agosti 23, 2024 na Leonard Mashabara na yametajwa faragha mbele ya Jaji Suleiman Hassan.

Wakili Emanuel Anthony, anayemwakilisha Mashabara akizungumza na Mwananchi amesema wanaiomba mahakama iangalie kumbukumbu na mwenendo wa kesi ya jinai iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Zabibu Mpangule wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Amesema kupitia tamko hilo, TLS ilisema watashirikiana na vyombo vya haki jinai ambavyo ni Polisi, waendesha mashtaka, Jeshi la Magereza na vyombo vya haki.
Wakili huyo amesema wanaiomba mahakama itamke kama ni halali kwa mawakili hao kuendelea kuwatetea washtakiwa.

Soma Pia: Watuhumiwa wa Ubakaji Kuwakilishwa na wakili wa kujitegemea

Wajibu maombi katika shauri hilo la marejeo ni TLS, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wengine ni mawakili Godfrey Wasonga, Meshack Ngamando, Boniventura Njeru na Sadick Omary wanaowawakilisha washtakiwa katika kesi ya jinai inayomuhusu binti ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa Dovya.

Wamo pia washtakiwa wa kesi hiyo, ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Wakili wa kujitegemea aliyeiwakisha TLS, Ezekiel Mwakabeje amesema shauri hilo limetajwa na Mahakama Kuu imewapa muda wajibu maombi kupeleka kiapo kinzani au kama wana pingamizi katika shauri hilo.

Amesema wamepewa muda hadi Jumatatu Agosti 26, 2024 kabla ya saa 3.30 asubuhi wawe wamewasilisha viapo hivyo kwa ajili ya kuangalia kama ni lini shauri litasikilizwa.

Akizungumzia kesi ya jinai dhidi ya Nyundo na wenzake ambayo pia inasikilizwa faragha, Ngamando amesema haikuendelea baada ya kufunguliwa kwa shauri hilo la maombi ya marejeo.
Screenshot_2024-08-23-21-09-46-014_com.instagram.android-edit.jpg
 
View attachment 3077561
Every one is innocent until proven guilt beyond reasonable doubt. Also all people have a right to representation, to enter plea of their own. The applicant in the original case meaning Republic must present it's case without flaws, prove beyond reasonable doubt that the said offence occured and it is against the penal code law. The judge just need to hear all sides and decide on the merits.
Watanzania acheni ujinga!!
 
Back
Top Bottom