Mahakama Kuu yapinga mgawanyo wa nusu kwa nusu wa mali kwa Wanandoa waliopeana talaka

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Mahakama nchini Kenya imetoa uamuzi muhimu kuhusu ugavi wa mali katika familia wakati kunapokuwa na talaka.

Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini ikiwemo pia katika mitandao ya kijamii wakati uamuzi huo umepitishwa huku kukiwa na visa vingi vya watu mashuhuri kutalikiana.

Katika uamuzi unaoonekana na wengi kama pigo kwa haki za wanawake nchini Kenya, Jaji wa mahakama kuu John Mativo amepinga wanandoa kugawana mali nusu kwa nusu wanapo achana kwa talaka.

Jaji Mativo amesema, wanandoa wanapoachana wana haki ya kuchukua kile walichochangia tu kifedha katika ndoa hiyo

Umauzi huo unaambatana na sheria ya ndoa nchini ambayo shirikisho la mawakili wanawake Kenya FIDA lmekuwa likifanya kampeni ifutiliwe mbali.

Kundi hilo linalotetea haki za usawa wa kijinsia limelalamika kuwa sheria hiyo inawanyanyasa wanawake, likidai kuwa kwa mara nyingi wanawake ndio hubeba mzigo mzito wa kulea watoto wakati talaka zinapopita.

Lakini jaji huyo leo itakuwa sio haki mtu kupata zaidi ya walichochangia wakati ndoa inapovunjika.

Kesi hiyo imefuatiliwa kwa makini na Wakenya wengi walioelezea hisia zao kupitia mitandao ya kijamii.

Mahakama imesema iwapo itaruhusu ombi hilo la FIDA, itatoa mwanya kuruhusu wanaoatafuta kujitajirisha kuingia katika ndoa kwa lengo la kujinufaisha.

Jaji amesema sheria haiwanyanyasi wanawake kwasababu umauzi huu pia utakuwa na manufaa na kuwalinda wale wanaofanya kazi kwa bidii na kuunda mali ya familia.
 
Mahakama imesema iwapo itaruhusu ombi hilo la FIDA, itatoa mwanya kuruhusu wanaoatafuta kujitajirisha kuingia katika ndoa kwa lengo la kujinufaisha.

Aisee kumbe ndio zingine ni kujijengea uchumi wa viwanda tu..
 
Safi sana Kenya

Wanawake wa nyakati hizi wanapenda sana ku play victims.....na wamefanya ndoa kama chanzo cha mapato kama sio kujitajirisha......

Akigundua uko vyema kiuchumi analazimisha ndoa kwa nguvu zote miaka kadhaa mbele anaanzisha visa ili umuache mgawane mali zako ambazo yeye alizikuta.....huu ni uonevu ambao umekuwa ukigharimu maisha ya wanaume wengi sana kimya kimya.......wengi wamekufa kwa machungu ya kutoamini wanachokiona.....

Hongera ziwaendee wanawake wapambanaji wanaopambana na waume zao kuleta maisha bora kwenye familia zao......

Laana ziwaendee machangudoa wanaotumia ndoa kama sehemu za kudhurumu mali za watu wakisaidiwa na sheria kandamizi.....dhidi ya wanaume

Emanuel Eboue
 
Hili ni pigo kubwa sana kwa wanawake, sana sana mwanamke atakacho ondoka nacho ni dressing table peke yake na makeup, Ambazo alinunua kwa msaada wa mme wake
 
Hili ni pigo kubwa sana kwa wanawake, sana sana mwanamke atakacho ondoka nacho ni dressing table peke yake na makeup, Ambazo alinunua kwa msaada wa mme wake

Lakini mwanamke unataka tugawane mali yangu pasu kwa pasu, inabidi pawe na maelewano ya jinsi ya kuachana sio nikimiliki mahoteli, vlabu na madaladala halafu nitongoze msichana na kumuoa, aanzishe visa baada ya miezi mitatu halafu mali yangu yote ipigwe pasu.
 
Ila ujue mwanamke akiolewa na ambaye hajaolewa ni tofauti...mwanamke akiolewa anakuwa passive kiuchumi kwa kuwa mara nyingi anakuwa mama wa nyumbani, na hata akifanya kazi hawezi kupata muda wa kazi sana akiwa ameolewa, asingeolewa mwanamke huyu angekuwa active zaidi kwenye utafutaji na angekuwa mbali..Siungi mkono kugawana mali nusu kwa nusu ila kusema aondoke na alichokipata akiwa kwako inakuwa haijakaa vizuri pia hasa ukute mwanaume ndio muanzilishi wa visa
 
Akothee and the likes hawawezi kufurahia huu uamuzi.

Siku hizi watoto wa kike wamefanya ndoa kua njia ya kujitajirisha.
Bravo Kenyans!
 

Hata mimi siungi mkono kwamba atoke bila chochote, maana mama wa watoto wangu lazima aishi maisha yenye hadhi na kwamba kuna siku nilimpenda bado kuna kiaina nitakua nampenda.
Lakini pia inategemea ugomvi wenu unahusu nini, labda umemfumania analiwa na mlinzi wa hapo nyumbani, hivyo apewe talaka na kuondoka na mali wakaishi na huyo mlinzi, inauma mpaka kwenye mifupa....
 
Inaweza kuwa na mantiki ila inapaswa kabla ya ndoa vilivyopo vijulikane na ikitokea ndoa kuvunjika vile vilivyopatikana wakati wa ndoa ndio vigawanywe
 
kwa tanzania hao wanaume wa kuwakuta na mali kiasi hicho ni wachache wengi huanza na wake zao au hata kama ukimkutana navyo sana sana ni nyumba moja na gari moja then vinaongezeka mkiwa wote, kwahiyo hii ikija huku kwetu hatutaathirika sana
 

Huo upassive ni wa kujitakia. Labda kama bwanaake kamzuia asifanye kazi. Lakini wanawake makazini wapo wengi tu ambao wameolewa.
 
Kuna mwanamama aliolewa na wote walikuwa wafanyakazi. Mshahara wa mke alikuwa anasaidia ndugu zake ikiwemo kuwalipia ada wadogo zake na kuwajengea nyumba wazazi wake. Kila alipohojiwa alidai yeye ameolewa hivyo jukumu la kuhudumia familia ni la mwanaume. Je katika hali kama hiyo ni haki kugawana pasu kwa pasu?
 
Hapana si kunyanyasa wanawake. Kifupi ni kuwa mwanamke apewe haki yake na Watoto wapate haki yao. Jukum la kulea Watoto linabaki kwa baba. Hivyo mwanamke anapewa tu kitoka Nyumba. Anaposema mwanamke ndo analea Watoto kwani anayetoka ni mke au mume? Kingine mwanamke anaweza kuolewa tena huko anakoenda hivyo kuruhusu kugawana sawa kunaleta bias Maana wanawake wengi hufanya ndoa km kitega uchumi. Ataachika ndoa hata mia ili tu kugawana mali
 
Ndio kusema Mzee Reginald Mengi akimuacha Jackline Ntuyabaliwe inabidi wagawane mali nusu kwa nusu...!!!!!?

Ndio huo ujinga ambao tukipinga tunaambiwa tunanyanyasa Wanawake!


Eti Ridhwan Siku akimtema Mam sap wake agawane nao milungula yote ya 2005-2015 Nusu Kwa nusu....
....Mack Donald , Mitsubishi ...Bangaldesha zao wenye akili hizo
 
Hii ngoma ikija bongo wanawake wamekula hasara!

Unakuta mwanamke ana kipato lakini ata chumvi ndani hanunui AF siku mkiachana mnagawana mali ambazo alikukuta Nazo na nyingine ulitafuta akiwepo bila ata yy kujigusa

Naitaman sana hii ikuje bongo
 
Hata kama anakuwa passive lkn pasu kwa pasu sio haki, ni dhuluma iliyo wazi. Kinachotakiwa ni kukokotoa asilimia anayoweza pata kwa nafasi yake kama mke; na mume pia hivyo hivyo anatakiwa kupata asilimia fulani ikiwa mke ndo alikuwa mtafutaji.
 
hahaha hapo anatakiwa apate asilimia mbili tu mkuu au sawasawa na alichochangia maana naye alikuwa anatafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…