Mahakama kuzuia kuvuliwa Ubunge ni kuingilia maamuzi ya Spika na ni kinyume na Sheria. Ingedili na uanachama wao tu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Leo Spika angekataa kuwavua ubunge akina mdee Chadema wasingeweza kwenda mahakamani kupinga uamuzi wake. Kupitia Sheria ya kinga kwa spika Basi mahakama isingeweza kabisa kuingilia maamuzi yake. Kunasheria zilitungwa ili kutumika kwa wapinzani tu. Mfano ile iliyoweka zuio la Spika kushitakiwa. Hii Sheria ni mbovu kuwahi kutokea.

Ila leo mahakama imemzuia Spika kufanya analisisi na kuja na mahamuzi. Imeona ifanye yewewe na iwavue ubunge yenyewe na sio Spika Tena Spika akiwa bado hajafanya maamuzi yoyote. Je, wakina Mdee walishindwa kabisa kupeleka malalamiko yao kwa spika na Spika kupitia vifungu na kutoa maamuzi sahihi?

Kwanini mahakama iingilie Kati shauri ambalo bunge bado halijatoa uamuzi. Leo ata mahakama ikiwavua uanachama akina mdee Spika akakataa kuwavua ubunge akina pa kumpeleka. Hivyo ni mtu asiyefikiria tu anaweza kuzani swala la covid linaweza kuamliwa kisheria. Kwani Sheria zetu NI za ovyo Sana na zinachanganya mno.

Bila kujali wamewasikiliza au kutowasikiliza utetezi wa kina Mdee, wanachama ndio walioamua kuuvua uanachama akina Mdee.

Kama maamuzi hayakuwa ya haki wajumbe ndio walitakiwa kufungua kesi kupinga kunyimwa fursa ya kupiga kura kwa Uhuru sio akina Mdee.

Kama wanachama hawawataki wanachama mahakama Inaweza kuwalazimisha?

Je, mahakama inatakiwa iamue uanachama tu. Uanachama ndio ukaamue Ubunge. Sasa mahakama kuweka zuio la Ubunge NI kichekesho sababu Kamati kuu na Baraza kuu waliamua juu ya uanachama wa kina Mdee na si Ubunge wao.

Mahakama ingeamua tu akina Mdee wasivuliwe uanachama Hadi kesi ya msingi isikilizwe na maswala ya Ubunge ikamwachia Spika aseme Sasa kuwa NI wanachama halali hivyo hawavui Ubunge.

Kifupi akina Mdee walitakiwa kufanya kila linalowezekana ili wanachama wajue hoja zao na waje wafanye maamuzi sahihi. Kupitia media na kila wanavyojua

Mahakama itakuwa ya ajabu ikisema uongozi wa chadema usio na Dola uliwatisha wajumbe wote ili wasifanye maamuzi.

Akina Mdee walipaswa wafikishe hoja kwa wajumbe mapema kupitia siasa. Kama mahakama Leo imemzuia Spika kufanya maamuzi ile Sheria ya Kinga ya spika ifutwe.
 
Mahakama imeshinikizwa na Magufuli; mtu ana roho mbaya amewanunua wapinzani.
 
Nchi hii uzalendo bado Sana, kuvunja katiba ya nchi Ni kosa kubwa Sana, nchi zingine kesho asubuhi bunge lingeshazungukwa na umma kuzuia wabunge feki kuzama mjengoni
 
Wananchi Wana maisha magumu halafu kundi la watu 19 wakisaidiwa na vyombo tivyovitegemea wanatumia rushwa kuliibia Taifa.
Rushwa ,rushwa rushwa ,rushwa ,rushwa ,rushwa ,kila mahali.

Lini mahakama inaamlia vyama kukaa na wanacha wasio wataka.

Basi mahakama itoe maamuzi mapema ili Taifa lisipata hasara.

Na kama rushwa haitatawala,je , hiyo 2025 wanayoisubiri waliendelea kuiba kudi zetu Kwa kujipeleka Bunge watarudisha Kodi zetu.?

Nawashauru Chadema watumie umma Sasa Kwa hali mbaya ya uchumi ULIOPO Dunia nzima kuanza kuhamasisha wanachama wote na wazalendo wa kweo sio wasaka Mali kama akina Tulia na Msajili kudai fedha zote walizohujumu wakina Mdee na wenzake Kwa kujipeleka Bungeni Kwa kinyume Cha Sheria za nchi na katiba ya nchi na Chama.

Waandae watu ili ikifika 2024 kuelekea 2025 yafanyike maandamano makubwa ya amani kushinikiza hao Wabunge wa Ndugai na Tulia akishirikiana na Msajili warudishe fedha za umma zilizotumiwa vibaya na kuhumu uchumi wa nchi.

Uzalendo Upo wapi kama hatuwezi kulinda fedha za nchi zisichezewe na kuibiwa na Genge la watu?

Ina maana hata wafanyakazi wa umma wakituhumiwa kuwa wameghushi na kuliibia Taifa basi wakimbilie mahakamani ili wazuie kusimamishwa kazi na waendelee kukalia ofisi za umma mpaka mahakama zitoe hukumu?? Kweli ndivyo mihimili inavyolinda maslahi ya Nchi? Bunge Gani linakaliwa na mihimili mingine Kwa kiwango hicho?

Waafrika Tuko sirious kweli na nchi zetu au Kuna kundi la watu wachache wapo Kwa ajili ya maslahi yao TU?

Spika haoni aibu kuwa anahujumu Taifa na kujenga mifumo ya kijinga kabisa kata Taifa hili maskini?

Yaani Kwa mfano Mhasibu wa Halmashauri ambaye ni WA Muhimli wa Serikali atuhumiwe Kwa kula mamilioni ya fedha za Maendeleo halafu Waziri wa Tamisemi atoe maelekezo kuwa asimamishwe kazi ili uchunguzi ufanyike halafu akimbilie mahakamani kuiopinga kuondolewa Kwenye ofisi hiyo na serikali umuache aendelee kuiba eti wanasubiri maamuzi ya mahakama?

Mhasibu huyo anasimamishwa kazi na anakwenda mahakamani akiwa nje ya ofisi ili itakapobainika kuwa alionewa mahakama inatoa haki yake ya kurudishwa na kulipwa Fidia.

Baada ya hii kesi kuisha hata kama ni miaka 100 ijayo watu wafuatao wanapaswa kushitakiwa Kwa kufoji na kuhujumu uchumi wa nchi Kwa kujipa Ubunge Kwa lengo la kujipatia Fedha:
(1) Halima Mdee na wenzake 19.
(2) Spika Ndugai aliyelazimishwa na serikali ajiuzulu.
(3) Spika Tulia
(4) Msajili wa Vyama vya siasa.
(5) Mwanasheria mkuu wa Serikali.

Hawa watu wamelisababishia Taifa hasara kubwa sana Kwa kudemka Kwa maslahi ya wachache badala ya maslahi ya umma.

Hapo ndipo tutakapoona kama mahakama ipo Kwa ajili ya maslahi ya umma au ya kakundi ka watu wachache kama lilivyo bunge.

Mahitaji ya Katiba Mpya ni muhimu sana sana.

Hata Chaguzi zijazo zitavurugwa bila katiba mpya na mahakama itatumika Kwa lengo la kulinda vitendo vya kihuni hasa kwenye chaguzi za serikali za mitaa,MADIWANI na Wabunge.

Wizi wa kura na ujinga Mwingine utafanywa Kisha watasema nendeni mahakamani mkapinge matokeo.
 
Ni uhuni mtupu unaofanywa na mihimili ya hili taifa ili kumfurahisha mkuu wao wa magogoni.
 
Bila kujali wamewasikiliza au kutowasikiliza utetezi wa kina Mdee, wanachama ndio walioamua kuuvua uanachama akina Mdee.

Kama maamuzi hayakuwa ya haki wajumbe ndio walitakiwa kufungua kesi kupinga kunyimwa fursa ya kupiga kura kwa Uhuru sio akina Mdee.

Kama wanachama hawawataki wanachama mahakama Inaweza kuwalazimisha?

Je mahakama inatakiwa iamue uanachama tu. Uanachama ndio ukaamue Ubunge. Sasa mahakama kuweka zuio la Ubunge NI kichekesho sababu Kamati kuu na Baraza kuu waliamua juu ya uanachama wa kina Mdee na si Ubunge wao.

Mahakama ingeamua tu akina Mdee wasivuliwe uanachama Hadi kesi ya msingi isikilizwe na maswala ya Ubunge ikamwachia Spika aseme Sasa kuwa NI wanachama halali hivyo hawavui Ubunge.

Kifupi akina Mdee walitakiwa kufanya kila linalowezekana ili wanachama wajue hoja zao na waje wafanye maamuzi sahihi. Kupitia media na kila wanavyojua

Mahakama itakuwa ya ajabu ikisema uongozi wa chadema usio na Dola uliwatisha wajumbe wote ili wasifanye maamuzi.

Akina Mdee walipaswa wafikishe hoja kwa wajumbe mapema kupitia siasa.
Kama mahakama Leo imemzuia Spika kufanya maamuzi ile Sheria ya Kinga ya spika ifutwe.
Kesi zote ambazo zinatakiwa yatolewe maamuzi ya mizengwe huwa anapewa jaji kipenzi . Sijui kaMa hukumu zake zinaweza kuwa reference popote.
 
Leo Spika angekataa kuwavua ubunge akina mdee Chadema wasingeweza kwenda mahakamani kupinga uamuzi wake. Kupitia Sheria ya kinga kwa spika Basi mahakama isingeweza kabisa kuingilia maamuzi yake...
Kawaida mahakama inao uwezo wa kumsikiliza mtu na kutoa maamuzi yake yasiyoweza kuingiliwa na chombo kingine chochote kile, na bila kujali mtu huyo ametoka wapi. Mahakama inao uwezo wa kumsikiliza mtu na kutoa uamuzi, hata kama mtu huyo ametoka mbinguni au kwenye sayari nyingine
 
Hapa
Kesi zote ambazo zinatakiwa yatolewe maamuzi ya mizengwe huwa anapewa jaji kipenzi . Sijui kaMa hukumu zake zinaweza kuwa reference popote.
Swala hapa mahakama inawezaje kuingilia Spika asifanye maamuzi
 
Kesi zote ambazo zinatakiwa yatolewe maamuzi ya mizengwe huwa anapewa jaji kipenzi . Sijui kaMa hukumu zake zinaweza kuwa reference popote.
Swala hapa mahakama inawezaje kuingilia Spika asifanye maamuzi
 
Wananchi Wana maisha magumu halafu kundi la watu 19 wakisaidiwa na vyombo tivyovitegemea wanatumia rushwa kuliibia Taifa.
Rushwa ,rushwa rushwa ,rushwa ,rushwa ,rushwa ,kila mahali.

Lini mahakama inaamlia vyama kukaa na wanacha wasio wataka.

Basi mahakama itoe maamuzi mapema ili Taifa lisipata hasara.

Na kama rushwa haitatawala,je , hiyo 2025 wanayoisubiri waliendelea kuiba kudi zetu Kwa kujipeleka Bunge watarudisha Kodi zetu.?

Nawashauru Chadema watumie umma Sasa Kwa hali mbaya ya uchumi ULIOPO Dunia nzima kuanza kuhamasisha wanachama wote na wazalendo wa kweo sio wasaka Mali kama akina Tulia na Msajili kudai fedha zote walizohujumu wakina Mdee na wenzake Kwa kujipeleka Bungeni Kwa kinyume Cha Sheria za nchi na katiba ya nchi na Chama.
Waandae watu ili ikifika 2024 kuelekea 2025 yafanyike maandamano makubwa ya amani kushinikiza hao Wabunge wa Ndugai na Tulia akishirikiana na Msajili warudishe fedha za umma zilizotumiwa vibaya na kuhumu uchumi wa nchi.

Uzalendo Upo wapi kama hatuwezi kulinda fedha za nchi zisichezewe na kuibiwa na Genge la watu?

Ina maana hata wafanyakazi wa umma wakituhumiwa kuwa wameghushi na kuliibia Taifa basi wakimbilie mahakamani ili wazuie kusimamishwa kazi na waendelee kukalia ofisi za umma mpaka mahakama zitoe hukumu?? Kweli ndivyo mihimili inavyolinda maslahi ya Nchi? Bunge Gani linakaliwa na mihimili mingine Kwa kiwango hicho?

Waafrika Tuko sirious kweli na nchi zetu au Kuna kundi la watu wachache wapo Kwa ajili ya maslahi yao TU?

Spika haoni aibu kuwa anahujumu Taifa na kujenga mifumo ya kijinga kabisa kata Taifa hili maskini?
Yaani Kwa mfano Mhasibu wa Halmashauri ambaye ni WA Muhimli wa Serikali atuhumiwe Kwa kula mamilioni ya fedha za Maendeleo halafu Waziri wa Tamisemi atoe maelekezo kuwa asimamishwe kazi ili uchunguzi ufanyike halafu akimbilie mahakamani kuiopinga kuondolewa Kwenye ofisi hiyo na serikali umuache aendelee kuiba eti wanasubiri maamuzi ya mahakama??
Mhasibu huyo anasimamishwa kazi na anakwenda mahakamani akiwa nje ya ofisi ili itakapobainika kuwa alionewa mahakama inatoa haki yake ya kurudishwa na kulipwa Fidia.

Baada ya hii kesi kuisha hata kama ni miaka 100 ijayo watu wafuatao wanapaswa kushitakiwa Kwa kufoji na kuhujumu uchumi wa nchi Kwa kujipa Ubunge Kwa lengo la kujipatia Fedha :-
(1) Halima Mdee na wenzake 19.
(2) Spika Ndugai aliyelazimishwa na serikali ajiuzulu.
(3) Spika Tulia
(4) Msajili wa Vyama vya siasa.
(5) Mwanasheria mkuu wa Serikali.

Hawa watu wamelisababishia Taifa hasara kubwa sana Kwa kudemka Kwa maslahi ya wachache badala ya maslahi ya umma.

Hapo ndipo tutakapoona kama mahakama ipo Kwa ajili ya maslahi ya umma au ya kakundi ka watu wachache kama lilivyo bunge.

Mahitaji ya Katiba Mpya ni muhimu sana sana.

Hata Chaguzi zijazo zitavurugwa bila katiba mpya na mahakama itatumika Kwa lengo la kulinda vitendo vya kihuni hasa kwenye chaguzi za serikali za mitaa,MADIWANI na Wabunge.
Wizi wa kura na ujinga Mwingine utafanywa Kisha watasema nendeni mahakamani mkapinge matokeo.
Kanuni za Chama

6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) (c) (d) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

Hapo tu kuna waliopewa taarifa kwa simu na bila kufafanuliwa makosa yao ili wapate muda wa kutoa utetezi.
Ukiendelea mbele...

6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.

6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au la.

Katika wote hakuna aliyepewa mashitaka kwa maandishi wala nafasi ya kutoa utetezi wala taarifa ya msingi ya mamlaka ya nidhamu. Mpaka hapo mwenendo mzima wa kuwafukuza uanachama ukawa batili.

Ukiwa na swali jingine uliza.
 
Hizo hoja zingepelekwa kwa spika. Spika akapitia na kutoa maamuzi. Kunasheria inayolinda madaraka na Kinga yake.
Pili mahakama isingejadili uanachama sio ubunge. Kwani akina mdee wameanda kumzuia Spika kufanya maamuzi mahakamani na si Chadema
 
Kumbe covid walichofanya sasa ni kwenda kupambana na spika asivurumishe rungu lake........kama mleta mada alivyosema mahakama ilitakiwa isitishe maamuzi ya wao kuondolewa uanachama na siyo ubunge kwa sababu ubunge wao ulikuwa haujasitishwa.
 
Na CHADEMA wao wamewavua uanachama na siyo ubunge
 
Back
Top Bottom