Mahakama na Polisi Shirikishi wa Godfather

Mahakama na Polisi Shirikishi wa Godfather

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
VYOMBO VYA HAKI VINAPOSHINDWA KUTOA HAKI NINI MATOKEO YAKE?

Nimepata kuandika hapa kisa cha Amerigo Bonasera na Godfather Don Veto Corleone mkasa maarufu katika kitabu cha Mario Puzo, "The Godfather."

Binti ya Amerigo Bonasera alitaka kubakwa na wahuni vijana wenzake aliodhani ni watu wema.

Binti alijitetea na wahuni wale hawakufanikiwa lakini walimpiga wakamvunja taya na kumuumiza vibaya usoni.

Amerigo Bonasera akakimbilia mahakamani kutafuta haki ya mwanae.

Hakuipata.

Vijana wale wahuni wale wabakaji wakaachiwa wakawa huru kuendelea na upuuzi wao mitaani.

Amerigo Bonasera akaenda kwa Mafia Don, Veto Corleone wa New York ya mwaka 1945 kutafuta haki yake.

Don Veto Corleone akamwambia Amerigo Bonasera, "Wewe umekwenda polisi na mahakama imekupa haki yako kwa nini hukuja kwangu toka mwanzo?"

Sasa hapa ni pa kushangaza kidogo.

Yaani Amerigo Bonasera kakosea kwenda mahakamani?

Ilitakiwa mashtaka yake ayapeleke kwa jambazi wa Mafia Don Veto Corleone?

Naam mashtaka yake sasa kayafikisha kwa Don Veto Corleone anasubiri mahakama yake itoe hukumu.

Kesi hii kwa Hakimu Don Veto Corleone ilikuwa nyepesi sana kwani ushahidi wote ulikuwa wazi.

Hapo hapo akaamuru askari wake mfano wa askari shirikishi wa huku kwetu wawatafute wale wahuni wabakaji wawaadhibu.

Amerigo Bonasera alifurahi sana akamuomba adhabu ya wale vijana wahuni wabakaji iwe kifo.

Don Veto Corleone alikataa akamwambia mwanae yu hai.

Siku ya pili hukumu ilipita.

Magazeti yale yale yaliyoandika stori ya vijana wale wahuni kuachiwa na mahakama wakaja na stori nyingine ya kuwa vijana wale wamepigwa vibaya sana jana usiku unaweza kusema wamegongwa na treni wako hospitali mahututi.

Watafiti na waandishi wa makala za uchunguzi wakagusia wakasema kuna uwezekano mkubwa kupita kiasi kuwa kuna mahakama nyingine ya hakimu muadilifu kapelekewa shauri lile na hakimu huyo lau kama si kutoka mahakama rasmi kaisikiliza upya ile kesi na katoa hukumu inayostahili.

Waandishi hawa wakaonya kuwa ni muhimu mahakimu wakatenda haki vinginevyo watawaponza watuhumiwa wanaowaachia ingawa wana makosa kufikwa na yale yaliyowafika vijana wale wahuni wabakaji.

Wazazi wa wale wahuni walipofika hospitali kuwatazama watoto wao waliona bora wangefungwa kuliko yale yaliyowafika kwa maana walikuwa hawatazamiki.

Wote walikuwa na vilema vya kudumu maisha.

Jamii zote zenye dhulma jamii hujitengenezea yenyewe njia zake za kujikinga na madhalimu.

Hizi mahakama zisizo rasmi huenda na kufanya kazi sambamba na mahakama za serikali.

Don Veto Corleone alifahamu kuwa alikuwa anashughulika na majambazi kwa hiyo kumshauri Amerigo Bonasera kurejea mahakamani kukata rufaa ni kazi bure.

Dawa ilikuwa kuwafungulia mbwa wake wakali Dobermann wakawashughulikie.

Picha Amerigo Bonasera anabusu mkono wa Don Veto Corleone kumshukuru kwa kuhukumu kesi yake kwa haki.



Screenshot_20201222-070812.jpg

Amerigo Bonasera na Don Veto Corleone

Screenshot_20201222-071338.jpg
Screenshot_20201222-071640~2.jpg
 
Sasa hivi nasoma kitabu cha GodFather revenge cha Mario Puzo na sasa Mkuu wa Mafia wa New York ni mtoto wa Don Veto Corleon, Don Michael Corleone
 
Sasa hivi nasoma kitabu cha GodFather revenge cha Mario Puzo na sasa Mkuu wa Mafia wa New York ni mtoto wa Don Veto Corleon, Don Michael Corleone
Kilembwe,
Utuwekee hapa lau kidogo unayosoma humo.
 
Nimetoka kusoma ya mbunge wa Sumbawanga huku nakutana na ulipaji kisasi uliotukuka. Funzo kubwa
 
"Bonasera! Bonasera!. Nimekufanyia nini kustahili dharau hii!? Umekuja bila kualikwa kwenye harusi ya binti yangu halafu......"
Mr._Big_Render.png
 
Labda Shekhe utujuze nani ni Don Corleone? Nani ni Bonasera nani ni mahakama na nani ni gazeti huni, ukilinganisha na yale unayoyambania.
 
Labda Shekhe utujuze nani ni Don Corleone? Nani ni Bonasera nani ni mahakama na nani ni gazeti huni, ukilinganisha na yale unayoyambania. N
Tangawizi,
Ingia Google fanya search utapata kila kitu.
 
Tangawizi,
Ingia Google fanya search utapata kila kitu.

I wanted to say in your world, You have taken the character of Don Corleone. What I do not know who is your Luca Brasi 😂😂😂😂😂
 
One day and that day may never come,i will call you to ask the service,until that day countinue to be my friend
 
Magazeti yale yale yaliyoandika stori ya vijana wale wahuni kuachiwa na mahakama wakaja na stori nyingine ya kuwa vijana wale wamepigwa vibaya sana jana usiku unaweza kusema wamegongwa na treni wako hospitali mahututi.
Hatari sana.
"Wewe umekwenda polisi na mahakama imekupa haki yako kwa nini hukuja kwangu toka mwanzo?"

Sasa hapa ni pa kushangaza kidogo.

Yaani Amerigo Bonasera kakosea kwenda mahakamani?
Ahsante sana kwa hii simulizi, Kuna jambo kubwa sana la kujifunza.
 
Back
Top Bottom