Una interest na kusoma vitimbwi vya Mafia? Soma kitabu kinachoitwa ''I Heard You Paint Houses'' kilichoandikwa na Charles Brandt hutajuta. Kinaelezea moja ya nadharia kadhaa jinsi Jimmy Hoffa alivyouawa. Jimmy Hoffa alikuwa ni kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi huko Marekani na alitoweka na mpaka sasa haijulikani ni nini kilimpata. Pia alikuwa kwenye genge la Mafia .Sasa hiki kitabu kinalezea jinsi alivyouawa na maelezo yanatoka kutoka kwa Mafia mwenzake alipohojiwa na Charles wakati anakaribia kufariki. Kweli Mafia ni ushirika wa hatari.