Mahakama pekee ndiyo imepewa mamlaka ya kutoa hukumu ya Kifo na si vinginevyo

Mahakama pekee ndiyo imepewa mamlaka ya kutoa hukumu ya Kifo na si vinginevyo

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Serikali kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama inawajibika kuwalinda raia wake kila wakati bila kujali hali zao au matendo yao. Haki ya Kuishi inakoma tu pale Mahakama inapotoa adhabu ya Kifo kwa mkosaji.

Ibara ya 14 hadi 17 ya Katiba ya Tanzania inalinda Haki ya Kuishi kwa Sheria namba 15 ya mwaka 1984 Ibara ya 6 inayotamka kuwa "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria".

Haki ya Kuishi pia ni Ibara ya 3 katika tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Ibara hii inasema Kila mtu ana Haki ya Kuishi na kwamba haki hiyo inalindwa na Sheria na hakuna Binadamu anayepaswa kunyimwa haki hiyo.
 
Nawaua wachawi wote, kwa upanga ukatao kuwili, nawaka nateketeza, nawapa za chembe, nawasambaratisha kuzimu.

Uwa wachawi wote wanaoua biashara yako, uwa wachawi wote wanaofanya watoto wako wawe wanakuwa wa pili kutoka mwisho kwenye mitihani.
 
Back
Top Bottom