Mahakama ya Dar es Salaam yaamuru mama na mwana kunyongwa hadi kufa kwa kumuua binti

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
1759330712026.jpg
Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewahukumu kunyongwa hadi kufa Sophia Mwenda mwenye umri wa miaka 64 na mwanawe Alphonce Magombola (39) baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya mwanafamilia wao.

Wawili hao walipatikana na hatia ya kumuua Beatrice Magombola, ambaye ni binti mkubwa wa Sophia, kwa kumchoma kisu chini ya titi mnamo Desemba 1, 2020 eneo la Kijichi, Wilaya ya Temeke.

Baada ya mauaji hayo, watuhumiwa walitupa mwili wa Beatrice maeneo ya Zinga, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Katika maelezo yake ya onyo yaliyorekodiwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Sophia alikiri kumuua binti yake ili kumzuia asitoe ushahidi katika kesi iliyofunguliwa na baba yake Beatrice. Mgogoro huo ulitokana na Sophia na Alphonce kuuza nyumba ya familia huko Mbeya bila kushirikisha wanafamilia wengine.

Nyumba hiyo iliuziwa Sh milioni 45, ambapo Sophia alipokea Sh milioni 12. Alimpa binti yake Rachel Sh milioni 1, ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi, huku Alphonce akichukua sehemu iliyobaki.

Hukumu hiyo imesomwa leo, Jumanne, Septemba 30, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio, ambaye alipewa mamlaka maalumu ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Hakimu Mrio alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, adhabu ya kosa la mauaji ni kifo cha lazima kwa kunyongwa.

“Kwa kuzingatia hilo, Mahakama inawahukumu Sophia na Alphonce kunyongwa hadi kufa. Hata hivyo, haki ya kukata rufaa ipo endapo mtataka kupinga hukumu hii,” alisema
Hakimu Mrio.

SOURCE

View: https://www.instagram.com/p/DPOxMiFiHwl/?utm_source=ig_web_copy_link
 
Mama anamuua mtoto wake? Jamii ya hovyo sana hii kwasasa.
Si mtoto wake wa kumzaa.
Beatrice ana mama yake, na baada ya mama yake kufariki, baba yake akaja kumuoa huyu mama muuaji. Baada ya baba kufariki ndio mama anataka kuuza hio nyumba ambayo kihalali ni urithi wa Beatrice.

Kiufupi mama muuaji anataka kuuza nyumba ambayo ni ya Bite
 
Rachel aliyepewa milioni moja ndie yupi tena mbona wanatuchanganya na hii habari?🤔

Halafu mbona wanasema baba ndie kafungua kesi?

Na mleta uzi kasema muwa Beatrice ndie mtoto wa kwanza wa huyo mama?🤔
 
Rachel ni mtoto wa mama muuaji ambae kazaa na huyu baba.
Ila huyu baba kamkuta mama muuaji tayari akiwa na Alphonce.
Kiufupi.
Beatrice huyu ni mama yake wa kambo.
Na Alphonce huyu ni baba yake wa kambo😄.
Mama Bite kafa na baba wa Alphonce nae kafa.
Sasa wakakutana ndio wakamzaa Rachel.

Baada ya baba Alphonce kufa, ndipo huyu mama muuaji akakutana na baba Bite wakapendana wakaoana na kumzaa Rachel
 
Imeandikwa msihukumu msije mkahukumiwa, hii kazi ya uhakimu hainifai kabisa aiseee!.
 
View attachment 3481990Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewahukumu kunyongwa hadi kufa Sophia Mwenda mwenye umri wa miaka 64 na mwanawe Alphonce Magombola (39) baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya mwanafamilia wao.

Wawili hao walipatikana na hatia ya kumuua Beatrice Magombola, ambaye ni binti mkubwa wa Sophia, kwa kumchoma kisu chini ya titi mnamo Desemba 1, 2020 eneo la Kijichi, Wilaya ya Temeke.

Baada ya mauaji hayo, watuhumiwa walitupa mwili wa Beatrice maeneo ya Zinga, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Katika maelezo yake ya onyo yaliyorekodiwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Sophia alikiri kumuua binti yake ili kumzuia asitoe ushahidi katika kesi iliyofunguliwa na baba yake Beatrice. Mgogoro huo ulitokana na Sophia na Alphonce kuuza nyumba ya familia huko Mbeya bila kushirikisha wanafamilia wengine.

Nyumba hiyo iliuziwa Sh milioni 45, ambapo Sophia alipokea Sh milioni 12. Alimpa binti yake Rachel Sh milioni 1, ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi, huku Alphonce akichukua sehemu iliyobaki.

Hukumu hiyo imesomwa leo, Jumanne, Septemba 30, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio, ambaye alipewa mamlaka maalumu ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Hakimu Mrio alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, adhabu ya kosa la mauaji ni kifo cha lazima kwa kunyongwa.

“Kwa kuzingatia hilo, Mahakama inawahukumu Sophia na Alphonce kunyongwa hadi kufa. Hata hivyo, haki ya kukata rufaa ipo endapo mtataka kupinga hukumu hii,” alisema
Hakimu Mrio.

SOURCE

View: https://www.instagram.com/p/DPOxMiFiHwl/?utm_source=ig_web_copy_link

Soon kwa muuza matairi na mama yake
 
Back
Top Bottom