Mahakama ya Juu yasitisha kwa muda uamuzi wa Seneti kumwondoa Gachagua na Uteuzi wa Naibu Rais mpya

Mahakama ya Juu yasitisha kwa muda uamuzi wa Seneti kumwondoa Gachagua na Uteuzi wa Naibu Rais mpya

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mahakama ya Juu nchini Kenya imetoa amri ya kusimamisha kwa muda uamuzi wa Seneti wa kuunga mkono kufukuzwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Jaji E.C. Mwita amechukua hatua hiyo akirejelea masuala makubwa ya katiba na umuhimu wa kulinda maslahi ya umma.

Kikundi maalum, kilichoteuliwa na Jaji Mkuu, kimepangwa kusikiliza kesi hiyo tarehe 24 Oktoba.

Itakumbukwa kuwa Bunge la Seneti nchini Kenya hapo jana Oktoba 17 lilipiga kura kwa kauli moja kumvua madaraka Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.

Maseneta waliendelea kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani licha ya kufahamishwa kuwa Gachagua amelazwa hospitali akiugua maumivu makali kifuani.

Mawakili wake wakiongozwa na Paul Muite waljiondoa katika mchakato huo wakihoji kuwa hawawezi kuendelea bila uwepo wa mteja wao bungeni.

Maseneta walipigia kura hoja zote 11 zilizowasilishwa dhidi ya Bw. Gachagua na hatimaye kuidhinisha hoja tano kati ya hizo.

==========

REPUBLIC OF KENYA
IN THE HIGH COURT OF KENYA AT NAROBI CITY
COURT NAME: MILIMANI LAW COURTS
CASE NUMBER: HCCHRPET/E565/2024
CITATION: RIGATHI GACHAGUA VS STATE LAW OFFICE AND SENATE AND 3 OTHERS

ORDERS (COURT D0CUMENT)​

THIS MATTER coming up for directions on the Notice of Motion and petition both dated 18th October 2024. before Honourable Justice E C MWITA AND UPON CONSIDERING the pleadings, supporting affidavits and attachments, I am satisfied that the petition and application raise monumental constitutional issues touching not only at the heart of a functioning constitution but also its fundamental tenets of the rule of law and human rights.

IT IS HEREBY ORDERED AS A MATTER OF URGENCY;

1. THAT the pleadings be served immediately and be responded to within 3 days after service.

2. THAT due the significance of issues raised in the petition and application, I certify this matter as raising substantial questions of law and public interest and therefore fit to be heard by a bench of uneven number of judges to be appointed by the Hon. The Chief Justice. The file be placed before the Hon. Chief Justice immediately for consideration in that regard.

3. THAT in the meantime, due to the issues raised in the petition and and application, and the urgency demonstrated, a conservatory order is hereby issued staying implementation of the resolution by the Senate upholding the impeachment charges against the petitioner, the Deputy President of Kenya, including appointment of his replacement, until 24th October 2024 when the matter will be mentioned before the bench to be appointed by the Chief Justice, for GIVEN under my hand and seal of the Honourable court this 18th Day of October 2024

Penal Notice: Take notice that any disobedience or non-observance of the order of the court served herewith will result in penal consequences to you and any other person(s) disobeying and not observing the same

SIGNED BY: HON. JUSTICE E.C. MWITA

  • Kenya.jpg

Pia, soma:
 
Ila mahakama za Kenya ziko so powerful,hii ni mara ya pili nashuhudia mahaka nchini Kenya ikipinga maamuzi ya serikali...
Hapa kwetu hata yule afande wa ulawiti mahakama haimwambii kitu na mahakama Haina Cha kumfanya ,hata asipo enda mahakaman itazungushwa na kupambwa weeeee ,yaan bas tuu
 
Hapa kwetu hata yule afande wa ulawiti mahakama haimwambii kitu na mahakama Haina Cha kumfanya ,hata asipo enda mahakaman itazungushwa na kupambwa weeeee ,yaan bas tuu
Daah mahakama za bongo
 
Mahakama ya Juu nchini Kenya imetoa amri ya kusimamisha kwa muda uamuzi wa Seneti wa kuunga mkono kufukuzwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Jaji E.C. Mwita amechukua hatua hiyo akirejelea masuala makubwa ya katiba na umuhimu wa kulinda maslahi ya umma.

Kikundi maalum, kilichoteuliwa na Jaji Mkuu, kimepangwa kusikiliza kesi hiyo tarehe 24 Oktoba.

View attachment 3128658
Mamayeezaoooooo senetaaa na mbwa wrnzake Russia shikamoooo
Nimesema rutoo atajamboo
 
Mahakama Kuu imesitisha azimio la Seneti la kuidhinisha hoja ya kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, lililofanyika Alhamisi, Oktoba 17.

Katika uamuzi uliotolewa Ijumaa, Jaji Chacha Mwita alibainisha kuwa ombi la Gachagua lilileta masuala muhimu ya kisheria na maslahi ya umma.

Jaji huyo alitoa agizo la muda la kusitisha utekelezaji wa mashtaka ya kumvua madaraka, ikiwemo uteuzi wa mrithi wake, hadi Oktoba 24, 2024, ambapo kesi hiyo itatajwa tena mahakamani.

Aidha, Jaji huyo alimwagiza Jaji Mkuu kuteua jopo la majaji kusikiliza kesi hiyo.

Kupitia mawakili wake, Gachagua aliwasilisha ombi la kumzuia Rais William Ruto kujaza nafasi hiyo. Alidai Bunge limeharakisha mchakato wa kumvua madaraka na kumteua mrithi wake kwa kasi isiyofaa.

Agizo la kusitisha utekelezaji limetolewa baada ya Bunge la Taifa kuidhinisha kwa kauli moja uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki, kuwa mrithi wa Gachagua. Kutokana na hatua hii mpya, uteuzi na kiapo cha Kindiki kitapaswa kusubiri hadi ombi la Gachagua litakaposikilizwa na kuamuliwa.

============For English Audience=======

The High Court has suspended the senate resolution to uphold former Deputy President Rigathi Gachagua's impeachment motion held on Thursday, October 17. In a ruling delivered on Friday, Justice Chacha Mwita cited that Gachagua's petition raised pertinent issues of law and public interest. He issued a conservatory order staying the implementation of the impeachment charges, including the appointment of his replacement until October 24, 2024, when the matter will be mentioned before court.The judge now directed the Chief Justice to appoint a bench to hear the petition.Through his counsel, Gachagua filed a petition seeking to bar President William Ruto from filling the position.

He cited the hurried nature in which parliament has rushed to conclude the impeachment process and replace him.The stay orders come after the National Assembly had unanimously approved the nomination of Interior CS Kithure Kindiki as Gachagua's replacement.

With the new development, Kindiki's appointment and subsequent swearing-in process will have to wait until Gachagua's petition is heard and determined.

SOURCE: CITIZEN DIGITAL
 
Back
Top Bottom