ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 475
- 353
Hivi rasimu ya katiba imesema chochote kuhusu Mahakama ya Kadhi wakuu? Mimi siku zote nilikuwa nafikiri Waislam wanataka kuwe na mahakama ya Kadhi, sasa nimeshangaa kuona tangazo kwenye gazeti la Daily News juzi kuna mtu anatakiwa kwenye mahakama ya kadhi ya Tanzania Bara kujibu shauri linalomkabili. Sasa nikajiuliza kama mahakama ipo, Waislam siku zote walikuwa wanataka nini? Kumbe Mahakama ya kadhi ipo na inafanya kazi.