Mahakama ya kadhi yawagawa waislamu

Mahakama ya kadhi yawagawa waislamu

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
Katika hali iliyonistaajabisha wanawake waislamu walikuja juu na kuivunjilia mbali hoja ya kuanzishwa mahakama ya kadhi kwa sheria ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hali hii ilitokea live jana wakati wa kutoa maoni mbele ya tume ya katiba maeneo ya Moshi bar. Ilianza pale ustaadh mmoja aliposimama na kutaka mahakama ya kadhi iingizwa katika katiba kwa kigezo kuwa mahakama za kiraia zimekuwa hazitendi haki hasa katika masuala ya ndoa na mirathi. Moto uliwaka pale alipojaribu kufafanua kwa kutumia mfano pale ndoa inapovunjika kwamba waislamu hawatendewi haki mahakamani. Kauli hiyo iliamsha jazba kwa wamama waislamu waliokuwapo pale na kuanza kutoa maoni kwa hasira wakiipinga vikali hiyo mahakama kwa vile itawafaidisha wanaume tu. Walilalamika kitendo kwamba mali wachume wote halafu ndoa inapovunjika waambiwe kuchukua walichokuja nacho, huku wakiwa wametumika wakachoka vilivyo. Walilalamika kwamba mfumo huo utachangia kuwanyanyasa mno wanawake wa kiislamu na hivyo mahakama ya kadhi haifai hata kidogo.

My take: Kumbe si makundi yote ya waislamu yanaafiki mahakama ya kadhi kama tunavyojaribu kuaminishwa.
 
Back
Top Bottom