Mahakama ya Kisutu yapanga Agosti 29, 2024 kusikiliza ushahidi wa kesi ya Boniface Jacob

Mahakama ya Kisutu yapanga Agosti 29, 2024 kusikiliza ushahidi wa kesi ya Boniface Jacob

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
GTusEVHWQAAg4tz.jpeg

GTusEVFWsAAex2d.jpeg
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti 29, 2024 kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha umma, inayomkabili meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (42) maarufu kama Boni Yai.

Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024 ni Godlisten Malisa (38) ambaye ni ofisa afya na mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
GTuh_EBWMAA4e4c.jpeg

Jacob ambaye ni mkazi wa Mbezi Msakuzi na mwenzake Malisa wanakabiliwa na mashtaka matatu, huku mawili kati ya hayo yakikabili Jacob pekee.

Uamuzo huo umetolewa leo Jumanne Julai 30, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo baada ya washtakiwa hao kusomewa hoja za awali( PH).

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom