Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mahakama ya juu zaidi nchini Malaysia imeeleza leo kwamba itasikiliza ombi la mwisho la Waziri Mkuu wa zamani Najib Razak la kubatilisha hukumu ya kifungo chake cha miaka 12 jela kwa tuhuma za ufisadi, na kuwa kuachiliwa kwake kunaweza kusafisha njia ya kurejea madarakani.
Mahakama hiyo imebaini kuwa rufaa hiyo itakayosikilizwa Alhamisi hii, ni ya mwisho kwa kiongozi huyo wa zamani, lakini ikiwa hatafaulu itabidi aanze kutumikia kifungo chake baada ya miaka mingi ya mvutano wa kisheria.
Najib Razak mwenye umri wa miaka 69 aliondolewa madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2018 kufuatia kashfa za kuhusika kwenye ufisadi wa mabilioni ya Dola. Alihukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani mnamo Julai mwaka 2020.