Mahakama ya Tanzania kuanza kutumia AI kwa ajili ya kurekodi mwenendo wa mashauri na hukumu

Mahakama ya Tanzania kuanza kutumia AI kwa ajili ya kurekodi mwenendo wa mashauri na hukumu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mahakama ya Tanzania imeanza hatua kubwa ya mageuzi ya kidijitali kwa kuanza kutengeneza mfumo wa kisasa unaotumia Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) kwa ajili ya kurekodi mwenendo wa mashauri na hukumu Mahakamani, hatua inayolenga kuongeza ufanisi, usahihi na kasi ya utoaji wa haki.

Akizungumza leo Februari 2, 2026 katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju amesema Mahakama inaendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili kuboresha utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema mfumo huo wa AI utawezesha kutafsiri na kuandika kwa wakati mmoja (Translation & Transcription) wakati wa usikilizaji wa mashauri Mahakamani, ambapo Jaji, Hakimu, Wakili, Shahidi na wadau wengine wanapozungumza, mfumo huo utatambua lugha inayotumika na kuiandika moja kwa moja kwa lugha iliyochaguliwa.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa changamoto ya kuchukua kumbukumbu kwa kuandika kwa mkono au kwa kutumia kompyuta, utaratibu ambao kwa muda mrefu umekuwa ukichelewesha mashauri, kuchosha wahusika na wakati mwingine kusababisha kupotoshwa kwa kumbukumbu za kesi.

“Mfumo huu utakapokuwa umeanza kutumika utaimarisha sana ufanisi wa utendaji wa Mahakama na kusaidia haki kutolewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi,” amesema Jaji Mkuu.

Aidha, amesema Mahakama itaendelea kuimarisha utaratibu wa kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao (online litigation), hatua itakayopunguza gharama za uendeshaji wa kesi na usumbufu kwa wadaawa, hususan wale wanaotoka maeneo ya mbali.
 
Haya ndiyo madhara ya kumiliki wasomi vilaza, mwisho waanze kuhukumu watu pasipo haki wakiulizwa wasingizie ni AI siyo wao, mipango ya mbogamboga ni ya hovyo sana.
 
Back
Top Bottom