Mahakama yaamuru Gazeti la The Citizen kumlipa aliyekuwa Bosi wa NHC, Nehemia Mchechu Bilioni 2

Mahakama yaamuru Gazeti la The Citizen kumlipa aliyekuwa Bosi wa NHC, Nehemia Mchechu Bilioni 2

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mahakama Kuu ya Tanzania imeliamuru gazeti The Citizen kumlipa fidia ya shilingi bilioni mbili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kwa kuchapisha habari zilizomshushia hadhi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam, ikielezwa kuwa gazeti hilo lilichapisha taarifa ambazo zilimtuhumu Mchechu juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma na kutumia maneno yaliyoshusha hadhi yake, huku wakidai walinukuu maneno ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, hayati John Magufuli alipokuwa akizindua mradi wa nyumba za NHC zilizopo Dodoma mwaka 2017.

Chanzo: Azam TV
 
Habari mbaya sana kwa uhuru na maendeleo ya sekta ya vyombo vya habari nchini.
 
Back
Top Bottom