Mahakama yaamuru Mwakinyo aitwe mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi

Mahakama yaamuru Mwakinyo aitwe mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeelekeza bondia maarufu nchini Hassan Mwakinyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi kufuatia kesi ya madai inayomkabili mahakamani hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo Amir Msumi baada ya Mwakinyo kukataa kupokea hati ya wito wa kufika mahakamani iliyowasilishwa kwake na msambaza nyaraka wa mahakama.

Mwakinyo alifunguliwa kesi ya madai na kampuni ya PAF Promotion, ambapo pamoja na mambo mengine iliwasilisha madai manane mahakamni hapo likiwemo la kuilipa kampuni hiyo TSH milioni 150 ikiwa ni madhara ya jumla baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.

Wakili anayeiwakilisha kampuni ya PAF promotion, Herry Kauki amedai kesi hiyo ilipangwa leo Novemba 13, 2023 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama bondia huyo amepewa wito wa kufika mahakamani.

Wakili Kauki alisema wao walipeleka wito serikali ya mtaa, lakini Mwakinyo aligomea wito wa kufika Mahakamani.

Pia walimtuma msambaza nyaraka za mahakama maalumu kwa ajili ya kupeleka viapo lakini Mwakinyo pia aligomea kupokea wito huo, hivyo msambaza nyaraka wa mahakama hiyo alikula kiapo kuelezea haya maelezo kuwa amepeleka wito lakini Mwakinyo amekataa kusaini wala kupokea wito huo.

Kutokana na hali hiyo hakimu Msumi alitoa amri kwa upande wa mlalamikaji ambaye ni kampuni hiyo kutangaza wito wa mahakama kupitia gazeti la Mwananchi, ukimtaka Mwakinyo kufika mahakamani hapo Novemba 20, 2023 ili kusikiliza kesi yake.

Chanzo: Mwananchi
1.Kaibiwa viatu airport.
2.Kauziwa viatu vinambana.
3.Kapangiwa pambano asilotambua undani wake.
4.Hababishwi na mapromota.
5.Hababaishwi na yeyote maana yeye ni Bora kuliko yeyote Tanzania.
6.Hakuna wa kumshauri maana ndondi alijifunza yeye binafsi na hakushauriwa na Mtu.

Kwa kauli hizo bado tunaona kuna mwanamichezo hapo?
 
Jamaa bonge la mjinga. Alafu hajijui kwamba yy ni mjinga na mpumbavu kwa wakati mmoja.
 
MWAKINYO BADO ATABAKI KUA BONDIA NAMBA MOJA TZ KAMA UKIWEKA CHUKI PEMBENI....
 
MWAKINYO BADO ATABAKI KUA BONDIA NAMBA MOJA TZ KAMA UKIWEKA CHUKI PEMBENI....
Huyu ni bondia mzuri kabisa na mimi nilikuwa shabiki wake.

Tatizo lilianza pale aliposahau viatu airport Uingereza na kuvaa viatu vya kubana. Baadae, kuna pambano alishinda kwa point bongo akasema sababu ni kuvaa bukta ya kubana, angevaa bukta nzuri angeshinda KO. Sasa unajiuliza, nani alimnunulia hiyo bukta. Maneno yake unaona yana ubabaishaji.

Mwakinyo atafute wataalamu wamuelimishe jinsi ya kuongea ili asionekane mbabaishaji, mwenye dharau na jeuri.

Haya, kwenye hili sakata la PAF Promotion, Mwakinyo alienda kwenye media kazungumza yake, PAF nao wakazungumza yao. Mwisho wa siku PAF wakaenda kushtaki bodi ya ngumi, na baadae mahakamani.

Sasa kwa nini Mwakinyo anakataa wito wa mahakama wakati mahakama ndiyo sehemu inayotafsiri sheria. Je, kukataa wito wa mahakama ndiyo suluhisho?
 
Lakini alishafungiwa
 
Back
Top Bottom