Mahakama yaamuru Safaricom kumlipa jamaa kipofu KSh6M kwa kumnyima kazi

Mahakama yaamuru Safaricom kumlipa jamaa kipofu KSh6M kwa kumnyima kazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mahakama Kuu jijini Nairobi imeamuru kampuni ya mawasiliano ya Safaricom kumlipa mwanamume kipofu KSh 6 milioni kwa kukosa kumuajiri.

Wilson Macharia alituzwa kima hicho cha pesa baada ya kushtaki Safaricom kwa kile alitaja kama kukiukwa kwa haki zake. Macharia alisema alinyimwa nafasi ya kuhudumu katika kampuni hiyo kwa msingi wa kukosa vifaa vya kumuwezesha kufanya kazi.

Macharia, hata hivyo alisema kuwa licha ya kualikwa kutia saini mkataba, alinyimwa kazi hiyo baada ya kuagizwa kutumia kipatakilishi yake. “Nimetambua kuwa sababu za mshtakiwa (Safaricom) zilitolewa kwa mlalamishi wakati imechelewa.

Mshtakiwa alifahamu fika kuanzia mwanzo kuwa kazi ya mlalamishi inahitaji mashine, japo walimpitiza kwenye utaratibu wote," aliamua Jaji Makau. Macharia alikuwa ametuma maombi ya nafasi ya huduma kwa wateja mnamo Agosti 2016 baada ya Safaricom kutangaza kuwa wazi.

Tangazo hilo lilimtaka Mkenya yeyote kutuma maombi bila kujali uraia, rangi, jinsia, kabila, ulemavu na umri. Macharia na watu wengine walemavu walikuwa miongoni mwa walioitwa kuhojiwa. Alipita mahojiano hayo ya kazi na kualikwa kutia saini mkataba wake wa ajira mnamo Julai 2017 lakini kampuni hiyo ilisema alialikwa kimakosa. Wakati alijaribu kutafuta sababu, kampuni hiyo ilidinda kuzungumzia suala hilo.

Tuko.co.ke
 
". . . Kampuni ilidinda kuzungumzia suala hilo."
Mambo ya kiswahili wakati mwingine yanafurahisha.
 
Back
Top Bottom