Mahakama yaanzisha matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence)

Mahakama yaanzisha matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence)

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Chanzo taarifa ya habari UTV/ TBC.
27/12/2022


Nimemsikia Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akizindua matumizi ya akili bandia katika mahakama zetu nchini.

Alieleza kuwa Matumizi ya akili bandia yatarahisisha utoaji haki kwani sasa computer inaweza kurekodi kile kinacho tamkwa papo hapo na Jaji au hakimu na kisha kutafasariwa na kutolewa.

Naamini hatua hii inaenda kuleta mabadiliko makubwa sana katika kutoa haki za wananchi, inamaa sasa akili bandia inaweza kutafasiri hukumu au maamuzi yatakayo somwa/tamkwa kwa lugha yoyote ile kulingana na mahitaji ya mwananchi, safi sana!

Ina maana sasa akili bandia inaenda kuondoa tatizo la upungufu wa Majaji na Mahakimu, akili bandia inaenda kufanya kazi ambayo ingefanywa na Mahakimu 5 inafanywa na akili bandia moja 1.

Hakika hii ni hatua kubwa sana, pongezi kwa Mahakama kwa kutumia tehama kikamilifu katika kurahisisha haki za wananchi.

Ushauri;
matumizi hayo yaanze mara moja lakini pia matumizi hayo yatumike kwa mahakama zote sio za mijini tu.
 
Siku utakayosikia kuwa JUDICIARY imekua huru na yenye kujitegemea kwa kuteua judges wake wenyewe ndio siku haki itapatikana, ila kwa sasa it's a NO,judge kuteuliwa na politician hakuna haki hapo,lazima atafanya kazi kwa mtazamo wa anayemlipa na kumlinda, CJ wote wa nchi hii kwangu hakuna aliyemfikia CJ NYALALI (rip),alikua very smart ingawa alifanya kazi kwenye mazingira magumu sana,ila hakutetereshwa na politicians kama hawa wa sasa
 
Hapo tayari lengo lishatimia, waliotoa pendekezo wameshapiga mpunga mambo mengine mtajua wenyewe.

Kwa mfumo wetu ulivyo, nnatilia shaka sana kama hivyo vifaa vitatumika. Hatujafikia kuwa na mahakama huru. Maamuzi yanaenda kulingana na wakuu wanataka yaende vipi.

Ni hatua nzuri Kwa kuanzia si haba.
 
Kwa hyo sie mahakimu/majaji ambao hatujaajiriwa mnategemea tukale wapi?
Jiongeze mkuu ingia kwenye uwakili wa kijitegemea, jisomee ili u specialize hasa kwenye corporate sector, international laws, na mwisho kutegemea kuteuliwa kuwa judge kwa fadhilia za politician, jaribu ile moral yako iwe juu hata unapoomba kwenye imani yako unakua free
 
kwa matumizi haya ya teknolojia naamini kabisa suala la upungufu wa Majaji na Mahakimu linaenda kwisha kabisa.
hatutegemei tena kusikia eti kuna upungufu wa majaji na mahakimu.
 
Mashine translation Kuna vitu ambavyo haiwezi kutafsiri vizuri mfano, mgaagaa anaupwa Hali wali mkavu, mchelea mwana kulia hulia yeye.
 
Back
Top Bottom