Mahakama yaizima Standard kumhusisha Charlene Ruto na tender ya sh. 2.8 bilion, Lakini Maswali ya Uniform bado hayajaisha

Mahakama yaizima Standard kumhusisha Charlene Ruto na tender ya sh. 2.8 bilion, Lakini Maswali ya Uniform bado hayajaisha

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Mahakama Kuu imezuia kwa muda Standard Group kuendelea kuchapisha au kusambaza madai yanayomhusisha Charlene Ruto, binti wa Rais William Ruto, na tender yenye utata ya takribani Sh2.8 bilioni ya sare mpya za polisi.

Amri hiyo ya Septemba 14 imetolewa baada ya Charlene kupinga machapisho ambayo, kwa mujibu wa kesi yake, yalimhusu moja kwa moja au kwa njia ya implication na watu au kampuni zinazohusishwa na procurement hiyo. Ni interim order, ikimaanisha kesi yenyewe bado haijaamuliwa kikamilifu.

Sakata hilo lilianza baada ya The Standard kuchunguza kampuni ya Nalitex Limited, ikisema baadhi ya taarifa zake za usajili zilikuwa na uhusiano na watu au biashara zinazohusishwa na First Family. Gazeti hilo pia liliripoti kuwa ofisi iliyosajiliwa ya Nalitex haikuweza kupatikana katika anwani iliyotajwa.

Lakini National Police Service baadaye ilikanusha kuwa Nalitex ilihusika na tender hiyo, ikisema kampuni iliyopata kazi ni Bedi Investments Limited, na kwamba Nalitex haikushiriki katika procurement, subcontracting wala kupokea malipo kutoka NPS.

Bedi yenyewe imesema imepewa kazi ya kutengeneza uniforms 58,701, lakini haijaweka wazi thamani kamili ya contract, huku ikikanusha madai kwamba mkataba wake wenyewe ni wa Sh2.8 bilioni.

Hapo ndipo suala linakuwa kubwa kuliko Charlene Ruto na Standard.

Ikiwa madai fulani ni ya uongo, serikali inaweza kuweka hadharani tender documents, bidders, lot values, evaluation records na contracts zote ili mjadala uishe kwa ushahidi?

Na kwa upande mwingine, mahakama inapolinda reputation ya mtu dhidi ya madai yasiyothibitishwa, tunahakikishaje pia kwamba injunctions hazizuii uchunguzi wa masuala halali ya matumizi ya fedha za umma?

Wadau, mwisho wa siku suluhisho bora si uvumi wala ukimya - ni kuweka procurement trail yote mezani.
 

Attachments

  • ruto-standard_0.jpg.webp
    ruto-standard_0.jpg.webp
    34.6 KB · Views: 19
Back
Top Bottom