Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Mahakama yakana kuandika Barua kuzuia mjadala wa Tegeta Escrow Account bungeni

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakati Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakichachamaa wakisema hawatakubali Bunge hilo kuingiliwa na mhimili wa Mahakama, Mahakama hiyo imejiweka kando na tuhuma hizo.

Sakata hilo lililotawala kikao cha Bunge hilo jana lilitokana na madai yaliyoibuliwa juzi na wabunge wa kupinzani unaoundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi.

Wabunge hao Tundu Lissu (CHADEMA), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Habib Mnyaa (CUF) waliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuwa wamepata taarifa za uhakika kuwa Mahakama imeandika barua ikiritaarifu Bunge lisijadili kashfa ya uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Wabunge hao, walisema kuwa hatua hiyo ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Bunge na kwamba lengo lake ni kutaka kukwamisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili wahusika wasichukuliwe hatua.

Msajili wa Mahakama Kuu, Amir Msumi, alipotakiwa jana na NIPASHE kuthibitisha kama Mahakama imeandika barua hiyo kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge kuzuia suala hilo lisijadiliwe kwa kuwa kiko mahakamani, alisema yeye na wasajili wenzake hawana taarifa kuhusu kuandikwa kwa barua hiyo.

"Labda unieleze hiyo barua imeandikwa na nani na lini, kama ni Jaji au Msajili nitajie jina lake ili iwe rahisi kufuatilia, lakini hadi sasa nimepekua kwenye kumbukumbu zetu sijaona barua hiyo," alisema Msumi.

Aliahidi kwamba jana angewasiliana na wenzake wa Mahakma ya Rufani kama kuna barua imeandikwa kutoka mahakama hiyo kwenda bungeni.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya serikali iliyothibitisha rasmi kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda Ofisi ya Spika wa Bunge.

Juzi Naibu Spika, Job Ndugai, alisema kuwa ofisi ya Spika haijapokea barua hiyo.

Hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akizungumza bungeni jana kuhusiana na madai hayo, hakuthibitisha wala kukanusha kama kuna barua iliyoandikwa na Mahakama kwenda bungeni kuzuia mjadala huo, zaidi ya kusisitiza itumike busara ili kuepusha mihimili hiyo kuingiliana katika majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Chanzo: Nipashe
 
Lazma wakanane mwaka huu, jaman kusema kwel namchukia sana pinda, yan kwanza linatisha kisura na ki ujambaz
Kama mna hakika kuwa barua hiyo ipo mbona hamjaiweka kwenye mtandao?
 
Wameanza kupoteana baada ya kuona maji yamezid unga na chombo kinaenda kuzama......sasa wanaogopa na wao kuwa sehemu ya kafala ...chezea kupewa ukweli live bila chenga.
ex-AG a.k.a TUMBIRI Bring back our money...
 
Last edited by a moderator:
Ni wapi amekanusha! Kasema hana taarifa labda jaji au mahakama ya rufaa. Hivyo hamna uhakika
 
Hakuna mahakama ya namna hiyon pengine ni mahakama ya kichaga au ukawa.

"Hakuna huo utaratibu wa kukufundisha wewe kuongoza Bunge, hivyo kama kuna barua imetoka mahakamani kwa jaji fulani naomba iwekwe mezani ili tumjadili huyo jaji, kama barua hiyo haipo basi tuendelee na shughuli zetu," alisema Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
 
leteni......... tumalize kazi haraka!
 
Ahsanteni Makamanda LISSU, MBATIA ...Naona hao wahuni wamepima upepo wakagundua ni wa kisulisuli....

Hapana Chezea UKAWA..
 
Hivi huyu Lizaboni ninani, ni Mtanzania? Manake sijawahii kuona hata siku moja akichangia hoja yeyote positively.

Si ajabu ukimwambia anakunya atakataa akuambie yeye hanyagi?

This is very serious. He is always negative in everything!
 
Back
Top Bottom