Mkuu kumbuka ile kesi ambayo walimu waliitisha mgomo nchi nzima, serikali ikakimbilia mahakamani, ilikuwa weekend, Jaji masatu alisoma hukumu hadi USIKU wa saa 2 hadi 4, na walimu waliambiwa kuwa mgomo wao ni batili, Jaji masatu alipohojiwa inakuwaje mahakama inafanya kazi hadi usiku na ni weekend, alijibiwa kuwa mahakama haina weekend na haki haina muda maalumu kuwa huu ni wa kazi au huu si wa kaxi.
Ha ha ha ha. Mwishon mwa para imeniacha hoi. Eti haki haina weekend, ni pale tu Mahakama inapojisikia kuwa leo haki itafutwe weekend!? Kama jibu ni hilo hapo kuna Double Standard!