Mahakama yakataa dhamana ya Lil Durk

Mahakama yakataa dhamana ya Lil Durk

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Timu ya mawakili wa Lil Durk iliwasilisha ombi mahakamani, wakitaka rapa huyo apewe kifungo cha nyumbani. Timu hiyo ilitoa ofa ya dhamana yenye thamani ya $3.3 milioni (sawa na takriban Tsh bilioni 7.8), ambayo ilijumuisha:

Nyumba mbili za Lil Durk zilizopo Georgia zenye thamani ya $2.3 milioni (Tsh bilioni 5.4) pamoja na fedha taslimu $1 milioni (Tsh bilioni 2.3), ambazo zingetolewa na Sony Music.

Hata hivyo, licha ya ofa hiyo kubwa, jaji alikataa kumwachia kwa dhamana.

Lil Durk anakabiliwa na shtaka la mauaji ya kulipwa (murder for hire), akidaiwa kuwatuma washkaji wake watano kumuua binamu wa rapa Quando Rondo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea mjini Los Angeles mwaka 2022.

1734076146540.jpg
 
Wanaamini akipewa dhamana atatumia nguvu, pesa na ushawishi alionao kuwadhuru, kuwatisha au kuwashawishi mashahidi... pia ile kutaka kutoroka kipindi anajua anaelekea kukamatwa inamfanya kuwa flight risk. Habari mbaya zaidi kwake feds wana ushahidi unaomhusisha na mauaji mengine.
 
Marapa kama kina future, kendrick, j cole wanasurvive kwa sababu hawana magenge ya kihuni na uhalifu kama hawa new rapaz in town sio?
 
Back
Top Bottom