Mahakama yalitia hatiani MwanaHalisi

Habari zilizonifikia punde tu zinadai Mahakama Kuu imelitia hatiani gazeti la Mwanahalisi kwa kumkashifu Bw.Rostam Aziz.

Mahakama inalitaka gazeti hilo limwombe radhi Rostam Aziz sambamba na kumlipa fidia ya shilingi za Kitanzania bilioni tatu.

Habari hizi bado hazijathibitishwa ingawa nimezipokea kutoka vyanzo vyangu vya kuaminika.

Wakuu hii nimeidakuwa kwa Mjengwa, kuna mwenye data zaidi?

Sorry wakuu kumbe ipo, tafadhali mod, ifuteni hii.. nimeshindwa kuifuta mwenyewe
 
Last edited:
Kama hii tarifa ni ya kweli nitarudia kuwakumbusha wana JF yale maelezo yangu niliyo andika hivi juzi ambayo ni kama ifuatavyo

8th May 2009, 01:49 AM
BABYLON

ROSTAM ni CCM na CCM ndio ROSTAM = ROSTAM ni SEREKALI na SEREKALI ndio ROSTAM ,

Palipo baki ni akili vichwani mwetu
 
kaka hii habari sio mpya tena ilisharushwa toka jana angalia thread inayosema kubenea na mwanahalisi washindwa na rostam
 
Hivyo ndio kusema kwamba yule tunayemwamini kwamba ana inside information regarding Rostam na Richmond ameshindwa...
Je wale wenzangu na mie wa makelele pwapwapwapwa...
 
Mh! kipigo kikubwa, si la kufurahia hilo kwani kubainea yupo kwa ajili ya kufichua mafisadi,inafaa tumuunge mkono sote na bakuli likipitishwa tuwe wa mwanzo... bt hofu yangu isije kuwa kubainea ana ugomvi binafsi na rostam... Namuomba kubainea asiwe na upande, coz i fil amebase baadhi ya sehemu kama kwa mengi... so awe yupo kwa ajili ya ukweli kwani hao wote ni mafisadi... USIDHARAU DAFU KWA MSIMU WA EMBE.....
 
Sijawahi kusikia kesi ya defamation ikiendeshwa kwa kasi ya aina hii hapa nchini. What does it mean? Sasa mkitaka kujua nguvu ya ufisadi ndiyo hii. Na bado tutashuhudia mengi zaidi. Kama hatutaki kupambana mafisadi watatumaliza! Amkeni jamani.
 
Habari zilizonifikia punde tu zinadai Mahakama Kuu imelitia hatiani gazeti la Mwanahalisi kwa kumkashifu Bw.Rostam Aziz.
zaidi?

Sorry wakuu kumbe ipo, tafadhali mod, ifuteni hii.. nimeshindwa kuifuta mwenyewe

Rwabu,
Vyanzo vyako vya habari ni dhaifu.
Umepata habari hizi punde?
 
Sijawahi kusikia kesi ya defamation ikiendeshwa kwa kasi ya aina hii hapa nchini. What does it mean? Sasa mkitaka kujua nguvu ya ufisadi ndiyo hii. Na bado tutashuhudia mengi zaidi. Kama hatutaki kupambana mafisadi watatumaliza! Amkeni jamani.

kaka acha kuzusha hapa bwana,nani kasema kuwa kesi imesikiliwa haraka, kwanza ndio ufanisi tunaotaka hapa nchini mwetu
 
Sijawahi kuona kesi ya defamation ikiendeshwa kwa kasi na hukumu kutolewa haraka namna hii. Sasa huo ndio ufisadi! Na bado tutashuhudia mengi zaidi.
 
Hivyo ndio kusema kwamba yule tunayemwamini kwamba ana inside information regarding Rostam na Richmond ameshindwa...
Je wale wenzangu na mie wa makelele pwapwapwapwa...

Ndugu yangu Kashehe, inawezekana MwanaHAlisi wana information za uhakika ama hawana, lakini kwa hii hukumu ya usikilizwaji wa upande mmoja, huwezi kufanya maamuzi uyasemayo. Tusubiri.

Kwa maoni yangu, hii kesi imewasilisha taswira ya nini kinachoendelea katika mfumo mzima wa mihimili yetu mikuu, yaani Bunge, Mahakama na Serikali na hata mhimil wa nne usio rasmi. Sipaswi kujadili hayo kwa sasa kwani kila mmoja humu ana taswira yake kuhusiana na kinachoendelea ndani na nje ya mihimili hiyo na wanaoumia ni WATANZANIA WOTE.
 
Maskini!!!huu ndio mwisho wa Kubenea. Kwahiyo akishindwa kulipa bil3 atafungwa?
Kesi madai hakuna kufungwa. Ni kulipa kama huna unafilisiwa. Kubenea akiandika barua kwa msajili wa makampuni na kudai, Mwanahalisi imefilisika, kesi imeisha, kesho yake anasajili gazeti jipya la 'Mwanahalisia' kazi inaendelea.
 
Huyu s.o.b vipi? Moderator, humu ndani ktk JF tumeingiliwa na watu wanaovuta. Inafaa kuwafanyia vetting ya nguvu. Hukumu tarehe 29 Aprili, siku 12 zilizopita hakuna hata gazeti moja la Rostam lisitoe hizo habari?

Hii hukumu ni ya kweli: Kila jambo hufanywa kwa mikakati. Walipanga waitoea baada ya tamko la serikali na huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuisafisha Richmond.

Jamaa wa mikakati na uwezo. Wanakaa na kupanga hawakurupuki. Walimmudu hadi Mkapa akasalimu amri. Wana serikali kamili nje na ndani ya uwanja. Ni HATARI kuliko munavyodhania. Mtu mmoja alisema, "Wasidhani Lowassa kalala, ni sawa na simba aliyelala kina Kubenea wanamchezea sharubu."

Kama unaangalia kwa makini utaona kuna:

AMRI KUMI ZA KIONGOZI WA KAMBO (SURROGATE LEADER) ROSTAM AZIZ.

1-Alianza mwenyewe "Surrogate Leader" Rostam Aziz
2-Akaja Sophia Simba na Mkuchika
3-Akaja Prof. Lipumba
4-Akaja Hamad Rashidi kwa swali la kumtega Pinda lakini yeye akauma na kupuliza
5. Akaja Dk. Shein kwa hotuba ya JK ya Mei Mosi ambayo tafsiri yake walikuwa nayo Mtanzania pekee na haikukanushwa
6. Akaja mwenyewe RA akaenda PCCB kwa "matarumbeta"
7. Akatoa tamko DCI tena kupitia Tanzania Daima la Chadema
8. Akaja DPP Feleshi katika Daily News
9. Akaja Mkuchika akiwa Busanda akisema tamko kesho (muandaliwe)
10.Tamko lenyewe zito akasoma Naibu Waziri, Bendera, tamko ambalo lilitoa kifupisho cha mchezo mzima kuanzia namba 1 hadi 9

Baada ya hapo sasa ndio amri ya mahakama inakuwa ruksa kuwa public ili sasa ionekane WAONGO HAOOOO!!!!! Kama Zuma watapeta!!!!
 
kaka acha kuzusha hapa bwana,nani kasema kuwa kesi imesikiliwa haraka, kwanza ndio ufanisi tunaotaka hapa nchini mwetu
Wana JF,
i) Nimezungumza na Bwana Saed Kubenea baada ya kuona taarifa hii na kutaka kupata ukweli. Nimemwuliza pia kama kwa manufaa ya Wana JF wanaotaka kufahamu ukweli ninaweza kupost ili tusiendelee na taarifa za kubahatisha.
a) Ni kweli kuwa Tarehe 30 April, 2009, Judge Makaramba, alitoa rulling katika kesi na 53/2008 kukashifiwa iliyowahusu, Rostam Aziz
vs
Editor Mwanahalisi,
Hali Halisi Publishers Ltd,
Printek Co.Ltd,
TSN (Tanzania Standard Newspapers Ltd)
Katika Rulling yake, Jaji Makaramba, alitupilia mbali ombi la Walalamikiwa la kupewa muda wa kuwasilisha utetezi wao (baada ya kuchelewa kuwasilisha majibu yao- Counter affidavit) kwa siku moja na baada ya kupokea pingamizi kutoka wa Wakili wa Rostam Aziz bwana Fungamtama. Walalamikiwa wote isipokuwa TSN wanatetewa na Kampuni ya Marando and Mnyere advocates Co.ltd. Kimsingi, walichelewa kujibu kwa sababu mhusika Mkuu yaani CEO wa Mwanahalisi na HaliHalisi Publishers Ltd alikuwa nje ya nchi kwa matibabu. Hata hivyo, Jaji Makaramba alitupilia mbali ombi hilo na wakati huo huo akakubali maombi (prayers) yote ya Rostam Aziz. Hata hivyo, TSN ambayo ilikuwa imewasilisha Counter Affidavit yao kwa wakati nao pia walikuwa hawakupewa nafasi ya kusikilizwa kabla ya Rulling hiyo, isipokuwa aliwatoa katika kulipa faini na gharama za kesi ( Sijaona Rullig yenyewe ningependa kuoiona ili niweze kutoa informed contribution hapa).
b) Baada ya Rulling hiyo, Walalamikiwa wote isipokuwa TSN wamekwisha kuwasilisha Mahakamani Notice of Intention to Appeal ( Court of Appeal). Proceedings tayari zimekwisha kupatikana, na ndani ya mwezi moja ( sheria inatoa siku 60 tangu siku proceedings zinapokuwa tayari) appeal itakuwa imewasilishwa Court of Appeal.

2: Wana JF nilipenda kuchangia kwa kutoa taarifa hiyo, ili wote tuwe kwenye wave length moja tunapochangia, na kuchangia hoja katika misingi yake sahihi bila jazba na bila ushabiki wowote. Hizi technicalities na mambo ya kawaida katika legal system, hivyo hakuna cha ajabu, tusubiri kuona Mahakama ya Rufani nayo itakuja na maamuzi yapi. Tufuatilie kwa karibu kuona haki inatendeka ama vipi.
 
Mkuu Halisi, Greetings!
Naomba ufafanuzi kwenye hayo maandishi niliyoyaweka kwenye alama nyekundu!
With due respect!
 
Hili ni pigo kubwa sana kwa Kubenea na MwanaHALISI.

Japokuwa kesi haijaisha, ili kuweza ku appeal inabidi Kubenea aweke dau chini kwanza, hela aliyohukumiwa aje nayo mkononi ndio mahakama ianze kusikiliza shauri la rufaa.

Rostam Aziz anashutumiwa na kila mtu kwamba ni jizi la kumwagiwa diesel, lakini yeye ana ujasiri, Wamarekani wanasema ana kende, anatangulia yeye mahakamani kusema haya, onyesheni nilimwibia nani, lini, wapi.

Mwenye vigezo, aliyemuona akiiba, na aje mbele. The most formidable dirt-digging journalist in the country, Kubenea, so far kashindwa mahakamani.

Next?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…