JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mahakama ya Rufani nchini Kenya chini ya jopo la majaji watatu imekataa kuingilia kati mchakato wa kuondolewa madarakani kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kupitia ombi la kuzuia mchakato huo.
Aidha, mahakama hiyo imesema mchakato huo utaendele kama ulivyopangwa bila kuingiliwa na mamlaka hiyo kwa sasa.
Mahakama iliyoketi mapema leo Jumatano Oktoba 16,2024 ilikataa kutoa maagizo ya kusitisha kesi ya kushtakiwa kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua katika Bunge la Seneti.
Majaji Erick Ogolla, Antony Mrima na Frida Mugambi wamesema hakuna suala lolote litakalomkuta Gachagua, iwapo Bunge la Seneti litaendelea na hoja ya kumtimua katika wadhifa huo.
Hata hivyo, Majaji hao wamesema uamuzi huo haumuzuii Gachagua kukata rufani kuupinga katika korti nyingine kama hatoridhika nao na pia mahakama bado inaweza kuamua matokeo ya mchakato wa Bunge.
Wakijibu uamuzi huo, timu ya wanasheria wa Gachagua imetaka kurekebisha ombi hilo kulingana na kile ambacho kinaweza kushuhudiwa katika Bunge la Seneti.