Mahakama Yamsamehe Kanja, Yamuonya Vikali Kuhusu Kudharau Amri

Mahakama Yamsamehe Kanja, Yamuonya Vikali Kuhusu Kudharau Amri

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
Mahakama Kuu imemsamehe Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja baada ya kumpata binafsi na hatia ya kudharau amri ya Mahakama iliyohusiana na vizuizi vya barabarani vilivyowekwa wakati wa maandamano ya Juni 25, 2026.

Jaji Patricia Nyaundi hata hivyo ametoa onyo kali kwa IG Kanja, akisema iwapo ukiukaji kama huo utajirudia, Mahakama haitasita kumhukumu kifungo cha gerezani

Kanja alifika mahakamani binafsi na kuomba radhi, akisema anajutia kushindwa kwake kuweka msimamo wake binafsi mbele ya Mahakama mapema. Pia alithibitisha kwamba amri za Mahakama zinawafunga wote, akiwemo yeye na Idara ya 'National Police Service, na kwamba polisi hawako juu ya sheria.

Alieleza kwamba vizuizi hivyo viliwekwa kutokana na kile alichokitaja kuwa hali ya usalama iliyokuwa ikibadilika kwa haraka, huku akisema hatua hizo zilionekana kuwa muhimu kulinda maisha na mali. Kanja alisema tangu wakati huo ametoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuhakikisha amri hiyo inazingatiwa katika mazingira kama hayo siku zijazo.

Mahakama imezingatia kujitokeza kwake binafsi, msamaha wake na ahadi ya kuhakikisha hakuna ukiukaji mwingine, ndipo ikaamua kumwachilia kwa sasa.

Hata hivyo, suala lenye uzito hapa ni kwamba Mahakama ilisema mwenendo wa Polisi ulikuwa umeathiri uhuru wa wananchi wa kuandamana kwa amani, na ikasisitiza umuhimu wa maafisa wakuu wa Serikali kuheshimu amri za Mahakama.

Je, unadhani IG Kanja alistahiki msamaha huo? Na Je, kuna uhakika gani kuwa Polisi hawatodhubutu kuzuia maandamano kwa kutumia vizuizi katika siku za usoni?
 
Back
Top Bottom