Feisal2020
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 1,113
- 2,656
Nyota wa rap wa Marekani, Young Thug, ameachiwa kutoka gerezani jana Alhamisi baada ya kukiri mashtaka ya kushiriki katika uhalifu wa genge, kumiliki silaha, na kutumia dawa za kulevya. Kesi hii inatajwa kuwa kesi iliyochukua muda mrefu zaidi katika historia ya Georgia.
Thug (Jeffery Lamar Williams) amekaa gerezani kwa siku zaidi ya na kufungwa gerezani kwa zaidi ya siku 900 tangu alipokamatwa mwaka 2022.
Waendesha mashtaka wa kesi hiyo walimtuhumu Young Thug kuwa kuongozi wa kundi la kihalifu ambalo pamoja na uhalifu mwingine, lilihusika kufanya mauaji katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Pia walidai kwamba YSL (Ambacho ni kifupisho cha jina la lebo ya mkali huyo ‘Young Stoner Life Records’ – pia ni kifupisho cha YOUNG SLIME LIFE, ambalo ni jina la genge la kihalifu la Atlanta lenye uhusiano na genge la Bloods.
Baada ya kukiri mashtaka Young Thug alipatiwa hukumu ya miaka 15 ya matazamio (probation) pamoja na muda ambao tayari alikua amekaa gerezani. Hakimu Paige Whitaker alimruhusu aendelee na maisha ya kawaida, lakini kwa masharti maalum, ikiwemo kufanya kazi za kijamii na amepigwa marufuku kuwasiliana na wanachama wa genge lake, isipokua kaka yake na Gunna.
Hakimu Whitaker aliongeza masharti kadhaa katika hukumu hiyo ikiwa ni pamoja na saa 100 za huduma ya jamii na kutoingia katika eneo la Atlanta kwa miaka 10 ya kwanza ya hukumu yake isipokuwa katika matukio maalum kama vile kuhudhuria harusi, mazishi, na kutoa elimu ya kupinga gangs – tukio analotakiwa kufanya mara nne kwa mwaka, na atatakiwa kuondoka Atlanta ndani ya masaa 48 baada ya shughuli hizo kuisha.