Mahakama yamwachia huru aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Nachingwea, Dkt. Mahadhi Mmoto na wenzake 11

Mahakama yamwachia huru aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Nachingwea, Dkt. Mahadhi Mmoto na wenzake 11

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
3,139
Reaction score
2,488
Mahakama ya Makimu Mkazi Lindi, imewafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mgombea ubunge ktk jimbo la Nachingwea, Dkt. Mahadhi Yusuph Mmoto na wafuasi wake 11 wa CHADEMA ambao walikamatwa wakati wa uchaguzi mwezi Oktoba 2020 kwa kuhusishwa na vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi.

Wote kwa pamoja watatakiwa kuripoti kituo cha polisi Nachingwea mjini Tarehe 16 Jumatatu ijayo.

Picha hapa chini ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Nachingwea Dkt. Mahadhi Mmoto (aliyechomekea shati la bluu) na wenzake 11 walioachiwa huru ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi

Hongera kwa serikali ya awamu ya 6 kwa kuimarisha maridhiano ya kisiasa

Mmoto.jpg
 
Haki ni lazima isimame,Mungu ametupigania wanyonge baada ya Kifo cha Magu (Mwendazake)
''Imeandikwa.

''Yanipasa mimi niondoke ..ili huyo roho wa kweli aje atawatia kwenye kweli yote na atanitukuza mimi........"
 
Mimi ni mwana mabadiliko kindakindaki. Lakini ukweli lazima tuuseme CHADEMA inahitaji kusukwa upya licha ya kwamba kiu yetu kuu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Haya maisha yaache tu...

Maenyekiti anaenda kuwekeza ulaya....wafia chama wanalala mahabusu.
Alikimbia jela, kama ulimsikia, anasema mlimfunga na kumfilisi akaunti zake akiwa jela. Kwa hio anajua ladha na adha ya jela
 
Mimi ni mwana mabadiliko kindakindaki. Lakini ukweli lazima tuuseme CHADEMA inahitaji kusukwa upya licha ya kwamba kiu yetu kuu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Anzisha chama chako .. unafiki haulipi
 
Mimi ni mwana mabadiliko kindakindaki. Lakini ukweli lazima tuuseme CHADEMA inahitaji kusukwa upya licha ya kwamba kiu yetu kuu ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Isukwe kivipi
Toa maoni yako
 
Back
Top Bottom